1 Fataawa Za Shaykh al-Imaam Ibn Baaz Imekusanywa Na Kufasiriwa Na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush 2 Swali: Kuna kundi la at-Twariyqah at-Tijaaniyyah wanakusanyika kila siku ya Ijumaa na Juma tatu na wanamdhukuru Allaah kwa Dhikr hii: "Laa ilaaha illa Allaah", na mwisho wake wanasema: "Allaah! Allaah!" kwa sauti ya juu. Sijui ni nini hukumu ya Kishari´ah kwa kitendo chao hichi? Imaam Ibn Baaz: at-Twariyqah at-Tijaaniyyah ni Twariyqah iliozushwa. Ni Twariyqah ya batili. Wako na mambo ya kufuru. Haijuzu kuifuata, bali ni wajibu kuiacha. Tunamnasihi yule aliyeshikamna nayo aachane nayo na ashikamane na njia ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Njia iliyopita Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na wakaipita maimamu wa Uislamu; kama mfano wa Imaam Maalik, Shaafi´iy, Abu Haniyfah, Ahmad, al-Awzaa´iy, Ishaaq Rahawayh, ath-Thawriy na wengine katika wanachuoni. Waliifuata njia hiyo, wakiwemo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Njia hiyo ambayo ni kumpwekesha Allaah na kumtakasia ´Ibaadah Yake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan, kwenda kuhiji Nyumba na kutii amri na makatazo aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii ndio njia aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama Twuruq asSuufiyyah ni wajibu kuziacha. Isipokuwa tu kile kitu ambacho kimeafikiana na Shari´ah. Wakiwa na kitu kilichoafikiana na Shari´ah, kitachukuliwa kwa sababu Shari´ah imekuja nacho. Ama kitu walichozua Suufiyyah kitaachwa. Na katika hayo ni kule kukusanyika kwao na kuleta Dhikr za pamoja: "Allaah! Allaah! Allaah!", au "Huu! Huu!". Yote haya ni Bid´ah na hayana asli. Ilikuwa inatakikana kusema: "Laa ilaaha illa Allaah", au "Subhaana Allaah, Ahmadulillaah, Laa ilaaha illa Allaah na Allaahu Akbar." Ama fujo za: "Huu! Huu!", au "Allaah! Allaah!", haya ni Bid´ah na hayana asli. Nakunasihi ewe ndugu muulizaji kuachana nao na ushikamane na njia ya Muhammadiyyah aliyokuja nayo Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nayo 3 ni zile Dhikr maarufu; "Subhaana Allaah, Alhamdulillaah, Laa ilaaha illa Allaah na Allaahu Akbar." Sawa ukiwa nyumbani kwako, Msikitini, njiani na kila mahali. Kama ilivyokuja kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Au wakakusanyika na kuanza kusema: "Allaah! Allaah!", au "Huu! Huu!". Yote haya nu munkari. Swali: Ninapokuwa katika muda wa hedhi husoma Qur-aan zile Suurah nilizohifadhi. Je, inajuzu kwangu kufanya hivyo? Imaam Ibn Baaz: Hakuna neno kufanya hivyo. Kauli yenye nguvu katika kauli za wanachuoni ni kuwa inajuzu kwa mwenye hedhi kusoma Qur-aan bila ya kuushika msahafu, asome kimoyoni kwa kuwa muda wa hedhi unakuwa mrefu na ni hali kadhalika kwa mwenye nifasi. Hakuna ubaya akasoma kimoyoni. Ama yule mwenye janaba, hapana. Mwenye janaba hasomi mpaka akoge, kwa kuwa muda wake yeye ni mdogo na anaweza kukoga. Hali kadhalika kwa yule mwenye hadathi ndogo. Asome kimoyoni na wala asisome katika msahafu mpaka atawadhe. Swali: Je, ni wajibu kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kila pale anapotajwa au hilo ni Sunnah? Imaam Ibn Baaz: Wajibu ni kumswalia pale anapotajwa jina lake (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Kutokana na yaliyothibiti kutoka kwake: "Ameangamia yule ambaye litatajwa jina langu kisha asiniswalie." 4 Hii ni dalili ioneshayo ya kuwa kumswalia ni wajibu kumswalia pale anapotajwa (´alayhis-Swalaat was-Salaam). 5 Swali: Ni ipi hukumu ya Twuruq katika Uislamu? Kwa kuwa kuna ambao nimewauliza wakasema kuwa ni Haramu, na wengine wakasema sio faradhi wala Haramu. Naomba jibu la wazi Allaah Akuwafikishe. Imaam Ibn Baaz: Swali haliko wazi. Ikiwa muulizaji anamaanisha Twuruq as-Suufiyyah ni munkari na Bid´ah; na baadhi yazo ni kufuru na zingine ni Bid´ah na sio kufuru. Kwa kuwa njia ambayo ni wajibu kuifuata ni njia ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa): َ ه ٰـ َ راطِ ي مُسْ َتقِيمًا ُ بعُو ه َ ِذا ص َ َّوأَن َ ِ فا َّت "Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni." (06:153) َ ه ٰـ َ ك َ َك َتابٌ أ ٌ ار ُبعُوه ُ ُنز ْل َناه ِ ذا َ م َب َو َ ِ فا َّت "Na hiki Kitabu (Qur-aan) Tumekiteremsha kilichobarikiwa, basi kifuateni." (06:155) ُخ ُ ها ُ ف ُ ما آ َتا َ ه َ ل ُ ع ْن ُ م الرَّ سُو فان َتهُوا َ م َ ما َن َو َ ُذوه َو َ ْك ُك "Na lolote (lile) analokupeni Mtume (Muhammad ( )صلى هللا عليه وآله وسلمbasi lichukueni, na (lolote lile) analokukatazeni, basi acheni." (59:07) Wajibu kwa Waislamu ni kufuata mfumo wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na waelekee katika njia yake na Dini yake. Anasema (Ta´ala): ُ م ُ نو َب ُذ ُ َغفِرْ ل ُ ب ْب ُ م ُ كن ُ ل إِن َّ فا ْ و َي َ ه ْ ُق ُ م اللَّـ ُب م ِ ت َ ه َ ُّون اللَّـ َ حب ْك ْك ْت ُك ِ ْعونِي يُح ِت "Sema (ee Muhammad )صلى هللا عليه وآله وسلم: “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu." (03:31) Njia ya Allaah iliyonyooka ni ile aliyokuja nayo Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na ndio njia waliyoneemeshwa kwayo. Kama ilivyo katika Kauli Yake (Jalla wa ´Alaa): ْ اط َ ر َ ِّر َ ْعم م ِ ْاه َ ت َ ِين أَ ْن َ اط الَّذ َ ِم ص َ د َنا الص ْ ْه َ المُسْ َتقِي ِ ع َلي 6 "Tuongoze katika njia iliyonyooka. Njia ya wale Uliowaneemesha" (01:06-07) Nao ni Mitume, maswadiki, mashahidi na watu wema. Kama ilivyokuja katika Kauli Yake (Ta´ala): ُّ وال َ ل ِّ ص ِّ وال ُ م اللَّـ ُن َّ وال ِ دي َ حس َ و َ ۚ ِين َ صالِح َ دَاء َش َ ين َ ق َ ِّين َ بي َ ْهم م َ ه َ ِين أَ ْن َ ع الَّذ َم َ ِك َ فأُولَ ٰـئ َ والرَّ سُو َ ه َ ع اللَّـ َو َ ِ ه َع ِ علَي ِ ِّن ال َّن ِ ِمن يُط ُ ً َ رفِيقا َ ِك َ أول ٰـئ "Na atakayemtii Allaah na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii, na asw-Swiddiqiyna na Mashahidi na (waja) wema, na uzuri ulioje hao kuwa ni rafiki (zake)." (04:69) Hii ndio njia ya sawa. Ama Twuruq as-Suufiyyah zina Shirki; kama kuwaabudu baadhi ya Mashaykh wao, kuwaomba msaada baadhi ya Mashaykh wao na yasiyokuwa haya katika Bid´ah zao nyingi. Kuna mmoja katika wao anasema: "Ni juu yako kujisalimisha kwa Shaykh huyu, kumpenda, na wala usimpinge kwa lolote, na uwe kwake kama maiti kwa mwoshaji." Twuruq zote hizi ni batili na potofu. Swali: Kulipitika majadiliano na maneno wakati wa ghadhabu baina yangu mimi na mke wangu nikawa nimemwambia mara tatu: "Kuishi kwako wewe na mimi ni Haramu" ilihali aliendelea kuishi nami. Je, nina kafara kwa hili? Imaam Ibn Baaz: Ni juu yako kwa hili kutoa kafara ya yamini. Kauli yako "Kuishi kwako na mimi ni Haramu" ni juu yako utoe kafara ya yamini kwa jambo hili na wala hulazimiki kitu baada ya hapo. Kwa kuwa hili hukumu yake ni yamini. Toa kafara ya yamini; nayo ni kulisha masikini kumi, au kuwavisha au kuacha mtumwa huru. Na kuwalisha maana yake ni kuwa utampa kila mmoja takriban 1,5 kg katika tende au chakula kingine chochote ambacho kimezoeleka mjini. Ukifanya hivi yatosheleza, Alhamduli Allaah. Na ni juu 7 yko Tawbah na Istighfaar. Kwa kuwa kujiharamishia Aliyomhalalishia Allaah. Muislamu haijuzu kwake Swali: Niliswali Dhuhr peke yangu, na katika Rakaa ya pili baada ya Suurat alFaatihah sikusoma Suurah nyingine katika Qur-aan kwa kusahau. Nikakumbuka kabla ya kutoa Salaam nikasujudu Sijda mbili za kusahau. Je, nina lolote katika hili? Imaam Ibn Baaz: Huna juu yako kitu. Na wala sio wajibu kuleta Sijda ya kusahau. Kwa kuwa kusoma Suurah nyingine baada ya al-Faatihah sio wajibu, muhimu ni kusoma al-Faatihah. Ama kusoma Suurah au Aayah baada yake ni jambo lililopendekezwa tu. Hivyo akiiacha mtu sio lazima alete Sijda ya kusahau au pindi atapoisahau. Swalah yake ni sahihi na wala haina neno. Swali: Kauli ya Allaah (Ta´ala): َ ِين ْ ه ْ ُق ُون َ ل َيعْ لَم َ والَّذ َ ُون َ ِين َيعْ لَم َ وي الَّذ َ ل ِ ل َيسْ َت “Je, wanalingana sawa wale wanaouja na wale wasiojua?” (39:09) Na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Wanachuoni ndio warithi wa Mitume (´alayhis-Swalaat was-Salaam)." Je, makusudio ni wanachuoni wa utabibu, kemia au wasiokuwa hao? Au makusudio ni wanachuoni wa Shari´ah? Imaam Ibn Baaz: 8 Makusudio kwa makubaliano ya wanachuoni wote ni ma´ulamaa wa Shari´ah, wanaochukua kutoka katika Kitabu na Sunnah. Wana fadhila kubwa na kheri nyingi. Ama kuhusiana na elimu ya udaktari, uhandisi na elimu zingine za dunia zinazofafana na hizo, ni elimu ambazo watu wao hukumu yao ni kiasi cha makusudio yao. Yule ambaye atajifunza uhandisi au udaktari ili awanufaishe Waislamu dhidi ya maadui wao, huyu ni mwenye kupewa ujira kwa kiasi cha nia yake. Hali kadhalika, kwa yule mwenye kusomea uanaskari, vita ili aje kuwanufaisha Waislamu, au akasomea uanajeshi ili makusudio yake ni kuwanufaisha Waislamu, huyu ni mwenye ujira na hukumu yake itakuwa kama ya wanachuoni wa Shari´ah. Ujira itategemea nia yake. Ama mwenye kusomea elimu ya dunia kwa makusudio ya kupata dunia ili aweze kula, au kupata kazi na kuishi, hili limeruhusiwa na hana juu yake kitu. Kwa kuwa Shari´ah imeamrisha kutafuta riziki. Lakini mtu huyu hawi kama yule aliyejifunza ili aweze kula pato la Halali na ajitosheleze na kuwaomba watu au awanufaishe Waislamu dhidi ya maadui wao, nia inatofautiana. Mwenye kujifunza kwa nia nzuri atakuwa ni mwenye ujira. Na mwenye kujifunza nayo ili ajiepushe na Haramu na achume pato la Halali, ni mwenye ujira. Na mwenye kujifunza nayo, hana makusudio yoyote ila tu ili apate kuishi, kula na kunywa, na makusudio yake sio kuwanufaisha Waislamu, yeye kajifunza nayo kwa maslahi ya kidunia tu, huyu kwake itakuwa inaruhusiwa tu. Swali: Nimeolewa na kijana na wala hakuniingilia baadae, na mimi kwa sasa nataka Talaka kutoka kwake kwa sababu nyingi, miongoni mwanzo:Ni mtu asiyekuwa na adabu na ni mjinga, wakati ninakaa nae katikatikatika kikao ananishutumu na kunitukana mbele ya watu. Hili ni jambo la kwanza. Jambo la pili, tokea tufunge ndoa imekuwa miezi mitano lakini hanihudumii jambo ambalo linalilazimu kwenda kuwaomba wazazi wangu pesa. Na jambo la tatu, ni kuwa ni mtu ambaye haswali na hata akiswali anaswali siku mbili na anaacha kwa muda wa mwezi. Nifanye nini? Nimeshamnasihi mara nyingi. Inajuzu kuomba Talaka au nitakuwa mwenye kupata madhambi? 9 Imaam Ibn Baaz: Ikiwa hali ni kama hii, kama ulivyotaja ewe dada muulizaji, anaswali wakati fulani na wala haswali kwa muda mrefu, huyu haijuzu kwako kubaki naye. Kwa kuwa kuacha Swalah ni kufuru kubwa kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni, hata kama hakupinga uwajibu wake. Ni wajibu kwako kuachana nae na wala haijuzu kwako kumwingilia wala kubaki katika ndoa, bali ndoa hii ni batili kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Ni juu yako [... sauti haiko wazi... ]. Na ikiwa hakukupa Talaka, ni juu yako kupeleka kesi hii mahakamani watatue ila hii. pamoja na kwamba, umesema ana mdomo mchafu wa kutusi na kulaani, hii ni ila nyingine. Lakini ila ya kuacha Swalah ni kubwa na iliyo wazi zaidi. Swali: Qadhiya ya mume kusafiri na kumuacha mke zaidi ya mwaka au miezi sita na kwamba hili ndani yake lina kitu kama mapungufu kwa upande wa mume, pamoja na kuwa baadhi ya watu wanalazimika kusafiri na kwa ajili ya kutoka kwenda kutafuta riziki. Anauliza hukumu ya hilo? Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya kwa mume kusafiri kutoka kwenda kutafuta elimu au riziki na wala hakuna mpaka wa (muda wa) safari yake, si kwa miezi sita wala kinyume na hilo. Lakini afanye vovyote itavyowezekana kusafiri pamoja nae ikiwa hali itaruhusu, hapo itatakikana kwake kusafiri nae ikiwa anaweza hilo. Ama ikiwa haiwezekani, amuache mahali ambapo ni pa amani na asafiri kutoka kwenda kutafuta elimu au riziki, na ajitahidi kuharakisha kumrudilia ili awe nae karibu na wala asicheleweshe muda. ´Umar bin al-Khattwab (Radhiya Allaahu ´anhu) aliweka mpaka kwa mume wa kubaki nje kwa kipindi cha miezi sita. Hiyo ilikuwa Ijtihaad yake. Akiweza kumjia baada ya miezi sita, miezi mine, miezi mitano au mitatu, hili ni jambo zuri. Na hali za wanawake zinatofautiana. Anaweza kuwa mahala pa amani na wala hakhofiwi juu yake kitu hata safari ikiwa ndefu, na anaweza kuwa 10 mahala ambapo si pa amani na anakhofiwa, katika hali hii inatakikana kujitahidi kumrejelea na kutazama amani ya hali yake ilivo. Jambo hili linatofautiana kutokana na hali ya mume na hali ya mke na hali ya nchi. Swali: Miaka mitano ya kabla nimeolewa na mwanaume mmoja hivi, na kabla ya ndoa nimemuuliza kuhusu Swalah akanambia kuwa haswali na akaniahidi kuwa ataanza kuswali baada ya ndoa In Shaa Allaah. Lakini kwa masikitiko makubwa, baada ya ndoa imedhihiri kuwa hatimizi ahadi yake na wala hatimizi Swalah za faradhi isipokuwa Swalah ya Ijumaa peke yake ndio anaswali Msikitini. Na daima humuombea kwa kuwa mimi namcha Allaah. Na nimesikia kuwa haijuzu kuishi na mtu ambaye ni kafiri mwenye kuacha Swalah. Je, hili ni sahihi? Imaam Ibn Baaz: Ndio, haijuzu. Swali: Kuna mwanamke alienda mahakamani kuomba Talaka kuachana na mume wake, wakamuuliza yuko wapi mume wako, akasema hayupo na wala sijui alipo. Mahakama wakawa wamemuomba alete mashahidi wawili wathibitishe hilo. Mashahidi hao wawili wakathibitisha ya kwamba bwana huyo hayupo na kwamba hawajui alipokwenda. Lakini wao (mahakamani) wanajua kuwa yupo katika mji huo na anafanya kazi, na ni wenye uhakika mkubwa kwa hilo. Mahakama wakawa wamempa Talaka. Baada ya hapo, akaolewa huyu mwanamke na mume wapili na mume wapili anajua maudhui hii kuanzia mwanzoni. Ipi hukumu ya mashahidi wawili, mwanamke huyu na mume wapili? 11 Imaam Ibn Baaz: Kesi hii wairudishe kwenye mahakama ambapo walihukumu, wawarejelee na wawabainishie hali ya sasa na mahakama iangalie hukumu yake. Masuala haya yanahusiana na mahakama, mahakama ibainishiwe hali ilivyo na kwamba mume yupo, walidanganya wakati walisema kuwa hayupo. Kwa vyovyote, kesi hii ipelekwe kwenye mahakama iliyohukumu mpaka waweze kutazama hukumu yake. Muulizaji: Shaykh, vipi kuhusu madhambi? Imaam Ibn Baaz: Mashahidi ikiwa walidanganya (kwa kujua), wako juu yao na madhambi, pamoja na manamke huyo. Muulizaji: Vipi na mume huyu wapili ambaye anajua hali ilivyo? Imaam Ibn Baaz: Na huyu pia ana madhambi. Na wala haijuzu kwake kumuoa naye anajua kuwa mume wake bado yupo, akamchukulia haki yake. Swali: Alimtaliki mke wake Talaka tatu, kisha akamrejea na kuishi nae miezi mingi. Kisha atamtaliki mara ya pili Talaka tatu, akabaki kwenye nyumba ya baba 12 yake miezi miwili. Kisha akamrejea tena bila ya ndoa upya na bila ya kuolewa na mume mwingine. Je, kumrejea kwake huku ni sahihi kwa hali hii au kuishi nae ni Haramu? Imaam Ibn Baaz: Haya ni masuala makubwa na ya khatari. Tunaona kuwa, huyu muulizaji na walii wa mwanamke warejee kwa Qadhiy walio naye huko Yemen, mpaka Qadhiy aweze kuangalia maudhui hii na atutue tatizo hili na awakhabarishe lililo la wajibu juu yao. Na wala haitoshi kulijibia hapa kwa njia ya idhaa. Swali: Ni upi usahihi wa mahala pa kaburi la Nabii Yuunus (´alayhis-Salaam) ni Iraaq? Imaam Ibn Baaz: Ama Yuunus (´alayhis-Salaam) haijulikani kaburi lake na wala hili halina usahihi. Bali makaburi ya Mitume wote hayajulikani,ila tu kaburi ya Mtume wetu Muhammad (´alayhis-Salaam) inajulikana, alizikwa nyumbani kwake Madiynah (´alayhis-Salaam). Hali kadhalika kaburi la Mtume Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alizikwa Palestina. Ama wasiokuwa hao wawili, wamebainisha wanachuoni ya kwamba hayajulikani makaburi yao. Na mwenye kudai ya kwamba hii ni kaburi ya fulani au fulani, ni muongo. Halina asli wala usahihi. Na mwenye kusema kaburi la Yuunus liko mahali fulani, halina asli. Inatakikana lijulikane hili. Swali: 13 Nimesoma Hadiyth katika baadhi ya vitabu vya Du´aa ya kwamba mwenye kusoma Suurat ad-Dukhaan usiku, watamuombea maghfirah Malaika 7.000. Upi usahihi wa Hadiyth hii? Imaam Ibn Baaz: Sijui usahihi wake. Haina asli kutokana na ninvyojua. Swali: Je, ni sahihi kwangu kufanya ndoa na msichana wa shangazi yangu au hapana? Imaam Ibn Baaz: Kufanya ndoa na msichana wa shangazi na mjomba, wote hawa inajuzu. Lililo la Haramu ni kumuoa shangazi yako au mama yako mdogo. Ama msichana wa shangazi yako na mtoto wa mjomba, hakuna ubaya wa hilo. Swali: Nilianza kupata ndoto nilipokuwa na umri wa miaka 13, na sikuswali wala kufunga ila nilipofikisha miaka 15, na hilo ni kutokana na ujinga wangu. Je, ni juu yangu kulipa Swalah na Swawm ya miaka miwili hii iliyopita au hapana? Imaam Ibn Baaz: Mtu akibalaghe miaka kumi na tatu kwa kuteremsha manii, kisha akaacha Swalah na Swawm kwa ujinga, hana juu yake kulipa. Kwa kuwa kuacha Swalah ni kufuru. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla). Mtu 14 aliyebaleghe kuacha Swalah ni kufuru kubwa kwa wanachuoni wahakiki, na hii ndio Ijmaa´ ya Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Na linatolewa dalili hilo na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalah, atakayeiacha kakufuru." (Hadiyth Swahiyh, kaipokea Imaam Ahmad na Ahl-us-Sunan) Kauli yake tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Baina ya mja na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah." (Kaipokea Muslim) Tawbah inatosha, maadam katubu kwa Allaah Tawbah ya kweli, inatosha na huna juu yako kulipa, si Swawm wala Swalah. Kwa kuwa aliyeritadi halipi kitu, na mwenye kuacha Swalah anazingatiwa kuwa ni mwenye kuritadi kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yake kutubu kwa Allaah upya na wala asilipe kitu. Achunge jambo hili katika Mustaqbal, kwa kuleta Tawbah ya kweli na kujilazimisha na ´amali njema. Swali: Nimemuapia mke wangu Talaka kwenye mkanda na nikamtumia nao, na kusema: "Ni juu yangu Talaka ikiwa sintoenda na nikachukua kiwango hichi kwa kaka yako, basi mimi nitakuwa nimekutaliki." Na baada ya hapo nikasafiri kwenda Misri na sikufanya lolote kuhusiana na yamini hii. Naomba faida. Imaam Ibn Baaz: Ikiwa kwa yamini hii, ulikusudia nafsi yako usifanye kitu hiki, au ulikusudia uweze kufanya kitu hiki. Ikiwa makusudio ni kuihimiza nafsi yako kufanya au kutofanya kitu, na makusudio haikuwa kufarakana nae na kumtaliki, hukumu ya hili ni hukumu ya yamini kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ama ikiwa ulikusudia kupita kwa Talaka ikiwa utafanya au 15 hutofanya, katika hali hii Talaka inapita ikiwa hukufanya. Ikiwa kama ulikusudia kupita kwa Talaka. Swali: Nilioa nami nilikuwa bado mdogo, na baada ya kuoa kwa takriban miezi kama mitatu nikwamwambia mke wangu mara nyingi: "Mimi sikutaki!". Waambie wazazi wako kuwa mimi sikutaki", pamoja na kuwa ni mke mwema. Na sasa sijui maneno niliyomwambia mke wangu huchukuliwa nimemtaliki au hapana? Kwa kuwa sikukusudia kumtaliki kwa kumwambia hivyo. Na ikiwa kama nimemtaliki, je nifunge nae ndoa upya kwa mara ya pili? Imaam Ibn Baaz: Maneno haya haiwi Talaka, uliyasema bila ya kukusudia hivyo, haiwi Talaka. Maadamu hakunuwia Talaka, si Talaka. Bado ni mke wake. Muulizaji: Je, ana kafara yoyote kwa hilo? Imaam Ibn Baaz: Hana juu yake kitu. Swali: Mke wangu alienda kwenye nyumba ya jirani mmoja nikakariri kumtaliki kwa sababu ya kwenda kwake bila ya idhini yangu. Nikamwambia chukua kila chako kwenye nyumba hii na mimi ni Haramu kwako. Lakini wazazi 16 wangu wawili hawakukubaliana na mimi, wakanambia: "Wewe ndiye utatoka kwenye nyumba hii na yeye (mke wako) atakaa na sisi". Sikutamka Talaka lakini nilimwambia tu: "Mimi ni Haramu kwako." Nimewauliza baadhi ya watu wakanambia kuwa hii sio Talaka na wala sina juu yangu kafara. Naomba unipe kauli ya sahihi katika maudhui hii. Imaam Ibn Baaz: Ikiwa hali ni kama alivyosema muulizaji, hakika juu yako una kafara ya Dhwihaar kwa kauli yako: "Mimi nimeharamika kwako". Ni kama mfano wa kusema: "Wewe ni kama mgongo wa mama yangu." Ni juu yako kutoa kafara ya Dhwihaar ikiwa hukukusudia Talaka kwa kusema kwako hivi. Ikiwa kwa hili hukukusudia Talaka, basi hukumu yake ni kama ya Dhwihaar. Kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yako kutoa kafara ya Dhwihaar, nayo ni kuacha mtumwa huru ambaye ni Muislamu, ikiwa hukupata utafunga miezi miwili mfululizo, ikiwa hilo ni gumu kwako na wala huwezi, utalisha masikini sitini ambao ni mafakiri. Kila mmoja utampa 1,5 kg ya tende, ngano au chakula chochote ambacho kimechozoeleka hapo unapoishi. Kila masikini mmoja utampa takriban 1,5 kg kabla ya kumgusa mke wako, kabla ya kumjamii. Huu ndio wajibu wako ikiwa hukukusudia Talaka. Ama uliposema: "Wewe ni Haramu kwangu" ikiwa ulikusudia Talaka, hili kutokana na kauli sahihi, ni kwamba ni Talaka moja itakuwa imepita ikiwa hapo mwanzo ulikuwa hujamtaliki, unaweza kumrejea kwa kusema: "Nimemrejea mke wangu, au mimi namrejea mke wangu, au namrejea mke wangu", au maneno mfano na hayo. Kwa kushuhudisha mashahidi wawili waadilifu ya kwamba umemrejea. Swali: Mimi nina rafiki kazini, ananambia ameoa tangu miaka kumi. Na mwanzoni wakati wa ndoa alikuwa haswali na sasa ameshakuwa na watoto watatu. Ndoa hii ni sahihi au hapana? Na kwa sasa - Alhamdulillaah - anaswali. Afunge ndoa upya? 17 Imaam Ibn Baaz: Ikiwa mke wake anaswali naye (mume) haswali, mke wake alikuwa ni Muislamu na mwenye msimamo, anaswali naye (mume) haswali wakati wa ndoa, ndoa hii si sahihi kwa wanachuoni wote. Kwa kuwa mwenye kuacha Swalah ni kafiri, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh: Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, atakayeiacha amekufuru." (Kaipokea Imaam Ahmad, Ahl-us-Sunan kwa isnadi sahihi kutoka kwa Buraydah (Radhiya Allaahu ´anhu) Na kapokea Muslim katika Swahiyh yake, kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Baina ya mtu na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah." Ni wajibu kufunga ndoa upya kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Na kuna wanachuoni wengine ambao wanaona kuwa hakufuru kwa hilo ikiwa anaamini kuwa (Swalah) ni haki na ni wajibu, lakini kaiacha kwa kuzembea na uvivu, wanaona kuwa ni muasi na ni kufuru ndogo, lakini si kufuru kubwa. Kutokana na kauli hii ya pili, itakuwa si lazima kufanya upya ndoa. Lakini kauli yenye nguvu inayosapotiwa na dalili, ni kuwa kufuru yake ni kubwa. Itakuwa ni juu yake kufanya ndoa upya kwa njia za Kishari´ah baada ya kutubia na Allaah Kumneemesha uongofu. Ama ikiwa mke wake alikuwa ni kama yeye kipindi cha ndoa, naye alikuwa haswali, ndoa yao hii itakuwa ni kama ndoa za Ahl-ul-Kitaab (mayahudi & wakristo) wengine. Ndoa yao ni sahihi na wala kutakuwa hakuna haja ya kufanya upya. Itakuwa ni juu yao wote wawili kutubu kwa Allaah kwa kuleta Tawbah ya kweli. Swali: Ipi hukumu ya madhiy yakiingia kwenye nguo, yaoshwe au yanyunyuziwe maji na kusafisha? Imaam Ibn Baaz: 18 Madhiy ni najisi, lakini najisi yake ni khafifu. Akinyunyuzia maji kwenye nguo yake, yatosha. Ama manii, ambayo ndio asli ya binaadamu, yanayotoka kwa nguvu na kwa shahawa na ladha, haya ni Twahara. Yakiingia kwenye nguo au mwili, utatwahirisha. Lakini, kuifanya nguo ikawa safi au kuiosha kabisa ndio bora zaidi. Swali: Ipi hukumu ya mwenye kuswali au kutekeleza ´Ibaadah yoyote katika ´Ibaadah naye mkononi mwake amevaa hirizi? Imaam Ibn Baaz: Hirizi ni Haramu na wala haijuzu. Na ni katika Shirki ndogo, na inaweze kwenda katika Shirki kubwa. Swalah yake ni sahihi, ikiwa hakuufanya moyo wake kuitegemea hirizi hiyo na akaitakidi kuwa inadhuru na kunufaisha. Hajatumbukia katika Shirki kubwa. Shirki ndogo haiporomoshi matendo (yote), isipokuwa Riyaa tu ndio inaporomosha ´amali iliyochanganyika nayo. Ama akivaa hirizi kwenye shingo yake au kwenye mkono wake... na atTamiymah baadhi ya watu wanaiita kwa majina mbali mbali kukiwmo jina la hirizi. Wanawavalisha watoto wao kuwakinga na kijicho, jini na huenda akavalishwa hata mgonjwa. Yote haya ni makosa na hayajuzu. Lakini halimzuii kusihi kwa Swalah yake kwa kuwa ni Muislamu, Swalah yake ni sahihi. Na hili ni kosa lake, kwa kuwa ni katika Shirki ndogo na makatazo. Na wala haiwi Shirki kubwa na wala haiwezi kwenda katika Shirki kubwa isipokuwa tu ikiwa ataufanya moyo wake kuitegemea (hiyo hirizi) na akaitakidi kuwa yenyewe ndio inaendesha, inaponya au inanufaisha yenyewe. Na hii ni I´tiqaad khatari yake ni kubwa, ni Shirki kubwa. Lakini mara nyingi Muislamu haamini hivyo, isipokuwa huwa anadhania kuwa ni katika kuchukua sababu. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Yeyote atakayevaa hirizi [au atakayejiambatanisha na kitu], basi Allaah Hatomtimizia matakwa yake kutimia kamwe. Na yule atakayevaa au kutundika chaza ndogo." 19 "Yeyote atakayevaa hirizi kafanya Shirki." Mtume kabainisha uharamu wa hirizi hii na uharamu wa kuivaa. Ni wajibu kwa Muislamu kutubu kwa Allaah ikiwa amefanya hili. Hali kadhalika muumini mwanamke atubu kwa Allaah kwa jambo hili na akate hirizi hii na mtu atahadhari nayo kabisa. Hata kama itakuwa ni hirizi iliyo na Aayah za Qur-aan. Ni wajibu kuikata. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kakataza hirizi na akaonya zote, na wala hakubagua hiriizi yoyote. Na ni kwa kuwa, kuvaa hirizi ya Qur-aan ni njia inayopelekea katika kuvaa hirizi nyinginezo. Ni wajibu kufunga njia zote za Shirki. Hii ndio nasaha zangu kwa kila Muislamu. Ya kwamba ni wajibu kwake kutahadhari na hirizi, na wala asiivae na kuitundika popote pale; si kwenye bega lake, kwenye shingo yake, mtoto wake, mkewake na kadhalika. Badala yake, ashikamane na Allaah na aombe kinga na hifadhi kwa Maneno ya Allaah yaliyotimia kwa shari ya Alivyoviumba na afanye sababu za Kishari´ah; Du´aa, dawa n.k., na vinatosheleza. Na wala hakuna haja ya hirizi. Huu ndio wajibu kwa kila Muislamu. Swali: Tatizo langu ni kuhusiana na mume wangu, ni mwanaume ambaye ana mapungufu katika Dini yake, haswali. Na pindi ninapomwita kuswali anakasirika na ananifanyia istihzai. Na anaendelea kuacha Swalah kwa hoja kuwa baba yake alikuwa haswali, hii ndio sababu na yeye haswali. Niliendelea na hali ya kumkumbusha na siku moja akanambia: "Ukiendelea kwa hali hii, mlango uko wazi", hapo ndio nilifika namuomba Talaka. Na mara ya pili ilikuwa takriban sababu hiyo hiyo. Akanambia: "Usiniongeleshi mpaka siku ya Qiyaamah". Ipi rai yako kwa mtu huyu na kwa maneno yake aliyosema kwa minasaba miwili, wa kwanza na wa pili? Je, huchukuliwa ni Talaka au nini? Na je, inajuzu kwangu kubaki nae katika hali hii? 20 Imaam Ibn Baaz: Mwanaume huyu haijuzu kubaki nae. Maadamu anaacha Swalah kama ulivyosema, kwa hilo anakuwa kafiri. Ikiwa baba yake naye haswali, kaiga kwake. Na wala haijuzu kumuiga kafiri asiyeswali, anatukana Dini, au anafanya kitu miongoni mwa vitu vinavyovunja Uislamu wa mtu au maasi katika maasi ya kumuasi Allaah. Watu wote hawa ni mamoja. Mwanaume huyu ni kafiri na kamuiga kafiri mwenzake kutokana na kauli yake. Na imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba kasema: "Baina ya mtu na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah." (Kaipokea Muslim katika Swahiyh yake) Na kasema (´alayhis-Swalaat was-Salaam): "Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, mwenye kuiacha amekufuru." Kauli yenye nguvu katika kauli za wanachuoni ni kwamba, mwenye kuiacha kwa kuzembea na uvivu ni kafiri, hata kama hakupinga uwajibu wake. Na ikiwa mwanaume huyu anapinga uwajibu wake, ni kafiri kwa Ijmaa´. Kwa hali yoyote, mwanaume huyu ni mwanaume mbaya na ni kafiri kwa kuacha kwake Swalah kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Haijuzu kwako kubaki nae. Bali ni wajibu kwako kuachana nae na wala usimpe kitu. Na kauli yake kusema kuwa mlango uko wazi, hii ni kinaya. Ikiwa amekusudia Talaka, anakusudia utoke kwa nia ya Talaka, itakuwa ni Talaka. Na ikiwa hakukusudia Talaka, itakuwa sio Talaka. Lakini kwa hali yoyote, hata kama hakukutaliki, haitakikani kwako kubaki nae. Bali ni wajibu kwako kumuacha na umuachie [... sauti haiko wazi... ], na watoto wako uwachukue na yeye (mume) hana haki ya (kubaki na) watoto kutokana na ukafiri wake. Wewe ndiye aula zaidi ya watoto wako. Ni mwanaume mbaya kwa kumkufuru kwake Allaah (´Azza wa Jalla). Huenda Allaah Akamsamehe. Akitubu nawe bado ungali ndani ya eda, akarejea, akatubu kwa Allaah na akajuta kwa aliyoyafanya na akaanza kuswali, hakuna ubaya kwako kurudi kwake na maadamu ungali ndani ya eda. Ama baada ya eda hapana (kurudi kwake), isipokuwa kwa ndoa mpya. 21 Swali: Sisi ni familia, tunakaa kwenye sinia moja wakati wa kula na hili ni jambo limezoeleka kwa ndugu - wanawake na wanaume sote tunakaa na kula kwenye sinia moja. Je, hili lina hukumu ya Kishari´ah inayokataza mchanganyiko? Mimi kwa hakika sina raha kwa hili, lakini ni mambo ya ada tu na kufuata kichwa mchunga ndio yameenea kwetu. Tufanye nini? Imaam Ibn Baaz: Hii ni ada chafu. Ni wajibu kuiacha. Na wala haijuzu kwa mtu kukaa na mwanamke ambaye sio Mahram wake, kama kwa mfano msichana wa ami yako, mjomba wako, shangazi yako. Ni wajibu kwa wanawake wawe upande wao kwenye sinia lao na wanaume wawe kwenye sinia lao upande mwingine. Ama kukaa na mke wako, mama yako, shangazi yako, msichana kukaa na mjomba wake na kaka yake hakuna ubaya. Lakini wanawake ambao wewe sio Mahram wao, haifai kwako kukaa nao kwenye sinia la chakula kimoja, isipokuwa wanawake hao wanatakiwa kukaa kwenye sinia la chakula kingine. Na wala mchanganyiko huu haijuzu jambo ambalo linapelekea mwanaume kugusana na mwanamke ambaye sio Mahram wake au kumtazama na yanayofuatia katika hayo. Mwili wa mwanamke wote ni ´Awrah (uchi). Hivyo haijuzu kwake kukaa na ambaye sio Mahram wake, akawa anaona anavyokula, uso wake n.k. Kwa vovyote, huu ni munkari na ni wajibu kuachana nalo. Na kila ada chafu ni wajibu kuiacha. Na ada ambayo inakwenda kinyume na Shari´ah na wala haijuzu kuitanguliza kabla ya Kishari´ah. Ni wajibu kuziweka ada kinyume na Shari´ah. Ile inayoafikiana na Shari´ah inakubaliwa na kubaki, na ile inayokwenda kinyume na Shari´ah ni wajibu kuiacha. Swali: Tunaomba kutoka kwenu kutuwekea wazi Aayah au Hadiyth ambazo zinaharamisha nyimbo. 22 Imaam Ibn Baaz: Ndio. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika Kitabu Chake kitukufu: ْ ْو َع َ و َي َّتخ ْ من َي ُه َّ ِن ال ۚ وا َب ٌُّهين ًز ُ َِك ل ُ ها َّ ِث ِليُض ِ يل اللَّـ ِ حدِي َ م َ ۚ أُو َل ٰـئ َ ِذ َ ْر عِ ْلم َ عن َ ل َ ال َ ري لَه َ اس َ وم َ ْه ِ ب ِ ذابٌ م ِ ه ِس ِ ن ِ غي ِ ش َت "Na katika watu (wako) wanaonunua maneno ya upuuzi (muziki, nyimbo n.k.) ili wapoteze (watu) njia ya Allaah bila elimu, na wanaichukukilia (njia ya Allaah) mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha." ُ ُ كأَنَّ فِي أ َع َ ِوإ ْو ْ ى مُسْ َت ِّ ف َب ُ ه آ َيا ُ ذا َ ۚ قرً ا َ ها َ برً ا ٰ َّول ٰ َت ْتل ُ ْشر ذاب أَلِيم ِ ذ َن ْي ِ علَ ْي َب َ ه َ ْمع َ ْم َيس َ ت َنا َ ى َ ْ َّكأَن ل ِ ه ِك "Na anaposomewa Aayah Zetu, hugeuka huku akitakabari kama kwamba hazisikii, kama kwamba kuna uzito (uziwi) masikioni mwake, basi mbashirie adhabu iumizayo." (31:06-07) Wamesema wanachuoni wengi, ya kuwa makusudio ya "... maneno ya upuuzi" ni nyimbo, ndio maneno ya upuuzi. Na wengine wakasema kuhusiana na Aayah hiyo, kunaingia ndani yake firimbi na matari na yanayofanana na hayo. Haya ndio maneno ya upuuzi yaliyoharamishwa. Na ni katika sababu ya kupotea kutoka katika Njia ya Allaah. Hakika ya moyo ukisibiwa na nyimbo unagonjweka, unakuwa mgumu na unapinda, jambo hilo likamkosesha kusikiliza Qur-aan. Jambo hilo likamsababishia moyo wake kupinda na kuihama kusikiliza Qur-aan, na badala yake ukajaa nyimbo na maneno machafu. Na imekuja kuhusiana na maana ya Hadiyth jambo ambalo linaonesha uharamu wa nyimbo. Katika hayo, ni yale aliyopokea al-Bukhaariy katika Swahiyh yake, ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Kutajitokeza katika Ummah wangu watu watakaohalalisha Zinaa, Hariri, Pombe na Nyimbo." Mtume (´alayhis-Salaam) kaelezea ya kuwa, kutajitokeza katika zama za mwisho watu ambao watahalalisha Haramu hii, kutokana na udhaifu wa Imani yao. Laa Hawla wa laa Quwwata illa biLlaah. Swali: 23 Sisi tunajua ya kwamba, kutumia mkono kwa kujitoa manii ni Haramu na ni jarima kubwa. Lakini vipi ikiwa mtu kalazimika kufanya hivyo kutokana na amri ya tabibu kwa maslihi ya kidawa au mengineyo, inajuzu kwake kufanya hivyo mwenyewe au kufanyiwa na mwingine? Imaam Ibn Baaz: Kujitoa manii ambako unatumiwa mkono ni jambo la Haramu na halijuzu. Na linaingia ndani ya Kauli Yake (Ta´ala): ْ م َٰ ء َ ِك ٰغ َ ُ عا َ ن ا ْب َت ُ ِك ون َ د َ ال َ فأُولَ ٰـئ َ ذل َ را َو َ ى َف ُه ِ م "Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka." (70:31) Anasema Allaah: ُ ح اف َّ ون ْ َى أ ُ ما َّ ِفإ ْ ك َ م َ َمل ٰ َعل َ م ُ غ ْي ُن ُن ُ ِين ِين َ ملُوم َ ر َ ت أَ ْي َ ما َ م أَ ْو َز َ ل َ ِظ َ م َ والَّذ َ ْه ْه ْه ْه ْه ِ وا ِ م لِفُرُو ِج ِج "Na ambao wanahifadhi tupu zao. Isipokuwa kwa wake zao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi." (70:29-30) Kisha Akasema: ْ م َٰ ء َ ِك ٰغ َ ُ عا َ ن ا ْب َت ُ ِك ون َ د َ ال َ فأُولَ ٰـئ َ ذل َ را َو َ ى َف ُه ِ م "Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio warukao mipaka." (70:31) Kujitoa manii linaingia ndani ya hili. Isitoshe, madhara yake ni makubwa ambayo wameyabainisha matabibu. Ni wajibu kutahadhari na hilo. Na hili ni Haramu kwa mwanamke na mwanaume wote wawili. Lakini, kukihitajika haja ya kufanya hivyo kwa ushauri wa matabibu atoe manii yake kutokana na madhara yaliyo nayo, hii ni dharurah na hakuna neno. Atafanya wakati wa haja. Ama kufanya hiyo ndo ikawa ada yako, kama wanavofanya baadhi ya wapumbavu, hili halijuzu. Ni wajibu kutahadhari. Ama hilo likihitajia haja ya kimatibabu na dawa, litakuwa halina neno. 24 Swali: Yatosheleza kwa mwanamke kuswali nyumbani kwake kwa adhaana peke yake, au kwa adhaana na ´Iqaamah? Hali kadhalika mwanaume akichelewesha Swalah yake na akaiswali nyumbani kwake, kinyume na wakati wake au katika wakati wake, inatosheleza kwake ´Iqaamah au ni lazima atoe adhaana na ´Iqaamah? Imaam Ibn Baaz: Ama mwanaume inatosha kwake ´Iqaamah, kwa kuwa kishasikia adhaana. Wakati wa kuswali atakimu tu. Ama mwanamke, hana juu yake ´Iqaamah wala adhaana. Ni juu yake kuswali bila ya ´Iqaamah wala adhaana. Swali: Kuko ambao wako katika Chuo Kikuu wanachukua elimu, lakini anataka kujua hukumu ya Uislamu, naye amechanganyika na wanawake, kwa kuwa masomo katika Chuo Kikuu hichi ni ya mchanganyiko, yaani ni wanaume na wanawake. Na wanawake wengi katika Chuo Kikuu hichi sio wenye kujisitiri na wanavaa nguo zinazoonesha. Imaam Ibn Baaz: Nasaha zetu kwa huu mwanafunzi ni kwamba asisome na wanafunzi wakike na wala asichanganyike nao. Kwa kuwa hii ni njia inayopelekea katika kufitinika nao. Ni juu yake atafute njia nyingine ya kujifunza. Ama kusoma na wasichana, hakika hii ni njia inayopelekea katika khatari kubwa. Ni wajibu kwake kutahadhari na hilo. Masomo ya mchanganyiko yana shari kubwa na ufisadi mkubwa. Na wala haijuzu kwa mtawala kulichukulia sahali. Bali ni wajibu kwa watawala masomo yasiwe mchanganyiko. Namna hii ndio inapaswa kuwa, watawala wa Waislamu ni wajibu kwao kufanya masomo ya wanawake yawe upande 25 wake pamoja na ulinzi na kuhifadhiwa, na masomo ya wanavulana yawe upande wake. Swali: Wakati fulani nina swali (Swalah za) faradhi mimi mwenyewe kwa kutokuwa na Msikiti ulio karibu na mimi. Je, inanilazimu kwangu adhaana na ´Iqaamah katika kila Swalah au naweza kuziswali bila ya adhaana au bila ya ´Iqaamah? Imaam Ibn Baaz: Sunnah ni wewe uadhini na ukimi. Hii ndio Sunnah. Ama kuhusu uwajibu, kuna tofauti kwa wanachuoni. Lakini aula na bora zaidi kwako ni wewe uadhini na ukimu, kutokana na ujumla wa dalili. Lakini, ni lazima kwako kuswali pamoja na Jamaa´ah (Msikitini)vovyote itavyokuwa, ukisikia adhaana Msikiti ulio karibu nawe, ni wajibu kwako kumuitikia muadhini na kuhudhuria pamoja na Jamaa´ah. Ikiwa husikii adhaana na wala huna Msikiti ulio karibu, Sunnah ni wewe uadhini na ukimu. Swali: Mimi ni mjane wa Kiislamu Alhamduli Allaah ambaye ninafunga na kuswali. Nilisibiwa na maradhi makubwa siku miongoni mwa siku katika Ramadhaan ambayo yalikuwa yanataka kuniua. Nikawa nimekula kutokana na ukubwa wa maradhi kisha nikalipa siku hii. Anauliza kama kula kwake (siku hii ya Ramadhaan) ana madhambi? Imaam Ibn Baaz: 26 Hana madhambi, bali ni mwenye kupewa ujira. Mtu akisibiwa na maradhi, na Swawm ikamkuwia kwake nzito inajuzu kwake kula na ni mwenye ujira kwa kuchukua rukhusa (ya Allaah). Anasema Allaah (Subhaanah): ُ ان مِن َ ُِدةٌ مِّنْ أَيَّام أ َ فر َس ٰ ع َل َ من َ َّ فع ر َخ َ ى َ َّريضً ا أَ ْو َ ك َف ِ كم م "Basi atakayekuwa mgonjwa miongoni mwenu, au yuko safarini (akafunga baadhi ya siku); basi (akamilishe) idadi (ya siku anazotakiwa kufunga) katika siku nyinginezo." (02:184) Na anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Hakika ya Allaah Anapenda kuchukuliewa (mambo ya) rukhusa Zake kama Anavyochukia kufuatwa maasi Yake (Aliyokataza)." Mtu akichukua rukhusa kwa kumtii Allaah na kufanyia kazi Aliyoyaweka katika Shari´ah (Ta´ala), ni mwenye ujira na hana madhambi. Wewe dada muulizaji huna dhambi juu yako kwa kula kwako kutokana na hali ya maradhi. Na ni juu yako kulipa na umekwishafanya hivyo Alhamdulillaah. Swali: Nilimtaliki mke wangu mara tatu. Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa Maghrib aliponambia maneno yaliyonikasirikisha nikawa nimemtaliki na (baadae) nikamrejea na kumrudisha nyumbani kwa kuwa ni mama wa watoto wangu wawili. Na baada ya siku kukatokea baina yetu magomvi, nikawa nimemtaliki. Akaingia kwangu na kuniomba nimrudi kwa ajili ya (maslahi ya) watoto. Nikamrudisha. Na baada ya siku kukatokea magomvi baina yetu kama ilivyokuwa katika hali ya kwanza na ya pili, nikamtaliki mara ya tatu. Naomba unifaidishe kwa hili. Imaam Ibn Baaz: Ni juu yako kurejea mahakamani au Muftiy aliye katika mji wenu waangalie suala hili. Na asli ni kuwa, baada ya Talaka tatu hakuna kurudiana. Lakini 27 apelekewe Qadhiy au Muftiy aangalie hilo. Ama ikiwa uko Saudi Arabia unaweza kuturejelea kwa kutuandikia, ili tuweze kukusaidia wewe na yeye kuyaangalia maudhui hii na tutazame uhakika, wewe, mwanamke na walii wake, mpaka fatwa iwe juu ya jambo la wazi ikiwa uko Saudi. aAma ikiwa uko katika mji mwingine na ikawa unaweza, rejea mahakamani au Muftiy wenu, na In Shaa Allaah Atawafikishwa kutoa fatwa inayoafikiana na Shari´ah. Swali: Akitalikiwa bikira kabla ya kuingiliwa, je itaandikwa katika ndoa yake ya mara ya pili kwa mume wa pili kuwa ni bikira au ni mwanamke ambaye kishaingiliwa? Imaam Ibn Baaz: Ni bikira. Ikiwa hakumwingiliani bikira. Ndoa mpya aliyofanya ikiwa hakuingiliwa, haimtoi katika ubikira wake. Maadamu (mume huyo) hakumwingilia, atabaki katika ubikira wake. Swali: Du´aa al-Istifaah (ya kufungulia Swalah) inasomwa katika faradhi na Naafilah, au ni katika faradhi tu? Imaam Ibn Baaz: Sunnah ni katika yote mawali, asome Du´aa al-Istifaah katika yote mawili faradhi na Naafilah. Hii ndio dhahiri ya Hadiyth ya Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). 28 Swali: Je, Duyyuuth ni yule ambaye anaelezea yanayopitika baina yake yeye na mke wake kitandani au ni nani Duyyuuth kwa mtazamo sahihi wa Kiislamu? Imaam Ibn Baaz: Duyyuuth ni yule ambaye anaridhia machafu ya mke wake, anaridhia kuchukuliwa mke wake, anaridhia mke wake kufanywa Zinaa. Huyu ndiye Duyyuuth. Ni yule ambaye anaridhia kuchukuliwa mke wake na kutumiwa, pasina kuwa na wivu wala kujali. Kwa kuwa na na Imani pungufu au kutokuwa nayo kabisa. Huyu ndiye huitwa Duyyuuth. Ama yule ambaye anaelezea hali yake na mke wake, haya ni maasi na anaweza kuwa fasiki kwa hilo. Lakini hawi Duyyuuth. Duyyuuth ni yule ambaye anaridhia machafu ya mke wake. Swali: Ipi hukumu kwa mwanaume ambaye ni Muislamu kumpa mke wake Talaka kwa kuandika jina la mwanaume mwingine naye (mke huyo) yuko katika dhimma yake ili wapewe pesa kutoka serikali? Imaam Ibn Baaz: Ni kama tulivyotangulia kusema, yote haya ni maovu na ni mali ya Haramu. Swali: Nataraji utanielekeza katika kitabu cha Hadiyth kizuri? 29 Imaam Ibn Baaz: Katika vitabu vizuri kwa mwanafunzi ni kitabu "Buluugh-ul-Maraam". Ni kitabu kizuri na ni chenye faida katika milango ya Ahkaam. Ni kitabu kizuri na chenye faida, "Buluugh-ul-Maraam" cha Haafidhw Ibn Hajar. Hichi tunatoa nasaha kihifadhiwe na khaswa kuzingatia yaliyomo katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Na kuna Hadiyth ambazo ni dhaifu lakini ni ndogo na kumebainishwa na kutanabahishwa hali zake. Kuna vitabu vingine vizuri ambavyo ni mukhtasari, "Umdat-ul-Hadiyth" cha ´Abd-ul-Ghaniy bin ´Abd-ul-Waahid bin ´Aliy al-Maqdisiy (Rahimahu Allaah). Kuna jumla ya Hadiyth nzuri. Kuna Hadiyth karimu 400 na zaidi kidogo zenye manufaa na faida. Lakini kilicho cha manufaa zaidi ni "Buluughul-Maraam". Kwa kuwa chenyewe ni chenye faida zaidi na kina Hadiyth nyingi. Swali: Tumejua kupitia barnamiji hii ya kwamba haipiti Talaka kwa mwenye hedhi na mwenye mimba. Je, ni kuwa haipiti kabisa au inapita baada ya Twahara? Imaam Ibn Baaz: Talaka ya mwenye hedhi haipiti kutokana na kauli sahihi (yenye nguvu) ya wanachuoni, tofauti na kauli ya jamhuri. Jamhuri ya wanachuoni wanaona kuwa inapita. Hali kadhalika kwa mwenye nifasi. Lakini kauli ya sahihi katika kauli za wanachuoni, na ndio waliokuwa wakifutu baadhi ya Taabi´iyn na Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na akaichagua Shayk-ul-Islaam bin Taymiyyah, mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim na kundi katika wanachuoni, kuwa Talaka hii haipiti. Kwa kuwa inakwenda kinyume na Shari´ah ya Allaah, kwa kuwa Allaah Kawekea Shari´ah kumtaliki mwanamke katika hali ya Twahara ya nifasi, hedhi na katika Twahara ambayo mume wake hakumjamii. Hii ndio Talaka ya Kishari´ah. Akimtaliki katika hedhi, nifasi au Twahara ambayo amemjamii, Talaka hii ni 30 Bid´ah na wala haipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni. Kwa Kauli ya Allaah (Jalla wa ´Alaa): َ ف َ ذا َإ ْ َّطل ِّ م ال ُق َ ء َّ طلِّقُوهُنَّ لِع َِّهن ُّ ََيا أ َ سا َ ن َي ُت ِ ِدت ِ ُّبي ِ ها ال َّن "Ee Nabii! Mtakapowataliki wanawake, basi watalikini katika wakati wa eda (twahara na si katika hedhi) zao." (65:01) Bi maana katika Twahara ya jimaa. Namna hii ndivyo walivyosema wanachuoni kuhusu (maana ya) "watalikini katika wakati wa eda." Wawe Twahara hawakuingiliwa au wawe na ujauzito. Hii ndio Talaka ya katika eda. Ama Talaka ya mjamzito wanachuoni wanaona kuwa inapita, na mwenye kusema kuwa haipiti kakosea. Talaka ya mjamzito inapita kwa wanachuoni, Talaka isiyopita ni ya mwenye hedhi na nifasi na Twahara ambayo mwanamke kaingiliwa na hakujadhihiri mimba yake. Talaka hizi (sampuli tatu) hazipiti kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni, kwa kuwa zinakhalifu na Shari´ah ya Allaah na vile vile ni katika hali ambayo haikuwekwa Talaka kama tulivyotangulia kusema. Na baadhi ya ´Awwaam wanastaajabu na kusema Talaka ya mjamzito haipiti, hili ni kosa. Hii ni katika kauli za ´Awwaam zisizokuwa na asli katika Shari´ah wala maneno ya wanachuoni. Mjamzito Talaka inapita. Ni wajibu kujua hilo. Swali: Baadhi ya migahawa na vinywaji vinaandikwa "haina-nguruwe", au "hainapombe". Je, mtu atosheke na maandiko kama haya na kuvitumiaau kuna neno? Imaam Ibn Baaz: Hakuna neno, maandiko haya yanatosha ikiwa ni katika mji wa mayahudi na manaswara, yanatosha maandiko haya. Asli ni kuwa, chakula (vichinjo) vyao ni Halali hata kama hakikuandikwa kitu. Na ikiwa kimeandikwa, inakuwa ni aula zaidi. Isipokuwa tu ikijulikana ya kuwa haya (waliyoyaandika) ni uongo na katika kitu hichi kuna nguruwe au kuna kitu kingine cha najisi, maandiko 31 haya yatakuwa hayana maana yoyote. Ikijulikana kwa dalili kutoka kwa waaminifu ya kwamba, huu ni uongo. Ama maadamu hakujajulikana kitu, asli ni kwamba inaruhusu na ni salama. Swali: Nimechumbia mwanamke wa umri wa miaka ishirini, na niliwahi kumsaidia kwa kumpa damu pindi alipokuwa mgonjwa kabla sijamchumbia. Je, inajuzu kwangu kumchumbia? Imaam Ibn Baaz: Damu haiathiri, sio kama kunyonya. Mwanamke kuolewa na mwanaume ambaye ana damu yake, au mwanaume kuoa mwanamke ambaye ana damu yake aliyompa wakati wa haja ya hilo, hili halina hukumu kama ya kunyonya. Mwanamke haharamiki kwake (mwanaume) wala (mwanaume) haharamiki kwake (mwanamke) kwa yaliyopitika katika kunufaishana kwa damu ambayo anaihitajia mgonjwa. Swali: Mimi naishi na ndugu zangu ambao hawaswali na mimi ninawapenda sana na wala siwezi kutengana nao kwa kuwa sina wengine badala yao. Je, inajuzu kuishi nao? Imaam Ibn Baaz: Ikiwa haswali hutakikani kuwapenda na wala hulazimiki kuwa na mapenzi juu yao kwa ajili ya Allaah, kwa kuwa watu hawa udhahiri wao ni ukafiri. Kwa kuwa mwenye kuacha Swalah anakufuru. Hivyo, ilikuwa haitakikani kuwapenda, bali uwachukie kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na 32 wala hutakiwi kuishi nao. Isipokuwa tu ikiwa kama ni jambo la kidharurah, hivyo utawanasihi daima, na kuwaogopesha Allaah, na kuwaambia "muogopeni Allaah enyi watu, swalini, zihifadhini Swalah, mcheni Allaah". Saidiana na aliye karibu yako katika ndugu zako; kama baba zao, babu zao, mama zao na mfano wa hao mpaka waweze kukusaidia katika kuwapa nasaha na kuwaelekeza katika kheri. Wakiendelea kuacha Swalah, watu hawa watakuwa hawana kheri yoyote. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa kasema: "Ahadi iliopo baina yetu na wao ni Swalah, atakayeicha basi amekufuru." Fanya vovyote utavyoweza usiishi nao, hata ikibidi kuishi katika nyumba ya wewe mwenyewe au baadhi ya ndugu zao wengine fanya hivyo. Hili ndilo la wajibu kwako kadiri na utakavyoweza. Swali: Mke wangu anaishi pamoja nami Saudi na anataka kuwatumia mzazi wake picha wanaoishi Misri ili apate utulivu. Na nimesikia Fatwa kuwa picha kwa ala ya picha ni Haramu. Je, hii ni dharurah? Imaam Ibn Baaz: Hii sio dharurah. Haifai kwake kutuma picha yake, sawa kwa mama yake wala asiyekuwa mama yake. Kwani hii sio dharurah. Amuandikie [barua], aongee nae kwenye simu. Alhamduli Allaah. Ama kutuma picha haijuzu. Swali: Je, ni sahihi ya kwamba jini linaweza kumwingia mtu na likamfanya akaongea kwa sauti yake? 33 Imaam Ibn Baaz: Ndio. Jini linaweza kumwingia mtu. Likamwingia kwa sifa maalumu na likamfanya mtu akatamka kwamambo, hujulikana sauti ya jini na ya sauti ya mtu. Hili ni jambo hutokea tangu zamani mpaka sasa. Hali kadhalika mwendawazimu. Aliyeingiwa na jini na mwendawazimu hutamka kwa maneno: "Nipeni kadhaa", "Fanyeni kadhaa" n.k., kwa sauti wanayoisikia watu isiyokuwa sauti ya mwanaadamu. Hili ni jambo ambalo hutokea, na mwenye kupinga hili kakosea. Jini humwingia mtu na kwa hili anakuwa kama mwendawazimu akili zake zinatoweka. Linapomtoka (jini hilo) na kutengana nae, akili zake hurudi. Swali: Anapomaliza mwenye kuswali Swalah yake na akataka kutoa Salaam, je aseme "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakatuh", kuliani kisha kushotoni." Au niseme "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi", tu? Na ni ipi hukumu ya mwenye kufanya hivyo kwa kuzidisha "... wa Barakatuh"? Imaam Ibn Baaz: Lililothibiti katika Sunnah ni kusema "... wa Barakatuh" tu, hii ndio iko katika Shari´ah, kusema "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaah" tu, hili ndilo liko katika Shari´ah. Nako ni kusema "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi", kuliani na kushotoni. Ama kuzidisha "... wa Barakatuh", wanachuoni wametofautiana. Na kapokea ´Alqamah (Radhiya Allaahu ´anhu) kutoka kwa baba yake kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema namna hii: "as-Salaam ´alaykum wa Rahmatu-llaahi wa Barakatuh". Lakini Riwaayah hii ya ´Alqamah ina tofauti. Kuna wanachuoni ambao wameisahihisha kutoka kwake, na kuna wanachuoni ambao wamesema kuwa imekatika (isnadi yake). Muislamu anatakiwa asizidishe, aula na bora zaidi aishie kwa kusema "... wa Rahmatullaah." Na mwenye kuzidisha kwa kudhani kuwa ni sahihi au hajui mambo haya, hakuna neno na Swalah yake ni sahihi. Lakini bora zaidi ni 34 kutozidisha. Hivi ndivyo walivyosema wanachuoni. Na kufanyia kazi jambo lililothibiti na lenye nguvu. Swali: Mimi nimemuoa mwanamke ambaye anaasi amri zangu na wala hanitii kwa kitu. Na daima anatoka nyumbani bila ya idhini yangu nakwenda kufanya baadhi ya kazi ambazo zimenifanya kunighadhibisha na kufikiria kumtaliki. Ikawa nimeandika karatasi ambapo nimeandika kuwa "nimekutaliki Talaka mbili" na nikamtaja kwa jina lake na la baba yake. Wakati huo nilikuwa nyumbani peke yangu na sikuwa na yeyote. Lakini baada ya hapo nikawa nimeichana hiyo karatasi na wala hakuna yeyote aliyejua kilichokipitika wala yeye. Na wakati huo ilikuwa ni kabla ya miezi mitano. Talaka imepita au hapana? Imaam Ibn Baaz: Ndio, zimepita Talaka mbili. Ukimtaliki kwa kuandika au kwa kumtakia, Talaka inakuwa imepita hata kama hukushuhudisha. Lakini umebaki na Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya hapo umebaki na Talaka moja. Unaweza kumrejea, na unaweza kumchumbia tena ikiwa kishatoka ndani ya eda. Muhimu ni kuwa kumebakia Talaka moja, ikiwa ulikuwa hujamtaliki kabla ya Talaka hii uliyoandika. Muulizaji: Kulikuwa kumeshapita miezi mitano kuanzia muda ule ambapo aliandika. Siatakuwa kishatoka ndani ya eda? Imaam Ibn Baaz: 35 Ndio, mara nyingi ni kuwa atakuwa kishatoka ndani ya eda kwa kupata hedhi au kwa miezi mitatu ikiwa ni eda ya mwanamke aliyokoma hedhi. Isipokuwa tu ikiwa kama ni mjamzito na hajajifungua, ni juu yake (aendelee) kukaa eda. Muulizaji: Vipi lakini kuhusiana na muda ule tangu aandike karatasi hiyo ya Talaka, ikiwa kwa mfano (alimtaliki) katika Twahara ambayo kamwingilia. Imaam Ibn Baaz: Kauli ya sahihi ni kuwa, ikiwa ni katika Twahara aliyomjamii au ilikuwa ni wakati wa hedhi, kauli ya sahihi ni kuwa (Talaka) haipiti. Tofauti na kauli ya wanachuoni wengi (wanaoonelea kuwa inapita). Swali: Hukumu ya mwenye kuacha Swalah na je anazikwa katika makaburi ya Waislamu? Imaam Ibn Baaz: Kuhusiana na mwenye kuacha Swalah kwamba atazikwa katika makaburi ya Waislamu, wanachuoni wametofautiana kuhusiana na hukumu yake. 1) Akiacha kwa uvivu na wala hapingi uwajibu wake, anaamini kuwa Swalah ni wajibu lakini akaacha kwa uvivu na kuzembea, kuna ambao wanaona kuwa hakufuru kufuru kubwa, bali ni kufuru ndogo. Na kwamba anazikwa pamoja na Waislamu wengine, kuoshwa na kuswaliwa. Hii ni kauli maarufu kwa kundi kubwa la wanachuoni. 2) Kauli ya pili ni kuwa, anakufuru kufuru kubwa. Na hii ndio kauli iliyo ya sahihi. Kutokana na hili, hatozikwa pamoja na Waislamu, bali atatafutiwa mahali afukiwe na asiachwe juu ya ardhi. Atazikwa kama ilivyo kwa makafiri 36 wengine. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth Swahiyh: “Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, atakayeiacha amekufuru." Na wala hakubagua yeyote, na wala hakusema ikiwa anapinga uwajibu wake (hakufuru). Na hii ni Hadiyth Swahiyh imepokea Ahmad na Ahl-us-Sunan kwa isnadi Swahiyh. Na Muslim kapokea katika Swahiyh yake, kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Baina ya mja na baina ya kufuru na Shirki ni kuacha Swalah." Shirki na kufuru inapokuja kwa sampuli hii inakuwa kubwa. Hii ndio kauli iliyo sahihi na yenye nguvu pamoja na kuwa kuna dalili zingine nyingi ambazo zinaonesha kuwa hata kwa mwenye kuacha Swalah kwa uvivu, hana lolote katika Uislamu. Swali: Mwanzoni wa mwaka katika ndoa yetu nilipatwa na khasira nyingi nikamuapia mke wangu Talaka, nikamwambia: "Mama yako akiingia hapa utakuwa ni mwenye kutalikika", na nilikuwa nimekusudia kumkataza asifanye hivyo na si Talaka. Na baada ya hapo mama yake akaingia na ndoa yetu ikaendelea mpaka sasa ni zaidi ya miaka 20 na nikazaa nae watoto na sikumuapia Talaka mara nyingne kwa kiasi cha muda wote huu. Ni ipi hukumu ya Talaka hii, imepita au hapana? Imaam Ibn Baaz: Kauli iliyo ya sahihi ni kuwa, Talaka hii hukumu yake ni ya yamini. Kwa kuwa hukukusudia kumtaliki, bali ulikusudia kum-kataza mama yake asiingie. Talaki hii hukumu yake inakuwa ya yamini kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Ni juu yako kukafiria yamini yako hata kama muda umekwishapita; kwa kulisha masikini 10 au kuwa-visha nguo, au kuachia mtumwa huru. Kama Alivyobainisha Allaah katika Kitabu Chake Kitukufu 37 katika Suurat-ul-Maaidah. Na kila masikini mmoja utampa 1,5 kg ya tende, mchele au visivyokuwa hivyo katika vyakula (vilivyozoeleka) katika mji, watapewa masikini 10. Au kuwakatia nguo, kuwapa kanzu au kikoi na nguo ya juu. Kufanya kwako hivi yatosha. Alhamduli Allaah. Na wala Talaka itakuwa haikupita na mke atabaki kuwa ni wako. Na wala haidhuru kwa muda wote huu mrefu. Isipokuwa tu ulikosea kwa kukawia kutoa kafara kwa muda wote huu mrefu. Ama kauli inayosema kuwa Talaka inapita (katika hali kama hii), ni kauli dhaifu. Kauli iliyo ya sahihi ni kuwa haipiti, maadamu makusudio yako ilikuwa ni kumkataza na kumzuia na haikuwa kumtaliki. Swali: Kuna siku nilihudhuria nyumbani, nikamkuta mke wangu amefanya kazi ambayo ilinikasirikisha. Nikamwambia "ukikaa nyumbani siku hii ya leo, nitakuwa nimekutaliki". Akawa ametoka siku hiyo hiyo na kisha akarejea baada ya wiki. Je, ametalikika au hapana? Na je, nina kafara yoyote? Imaam Ibn Baaz: Ikiwa makusudio ilikuwa ni kumkataza kubaki siku hiyo na usiku wake tu, hakupiti kitu, kwa kuwa alitoka na hakurudi isipokuwa baada ya wiki. Ama kama makusudio yako ilikuwa ni kutengana nae, makusudio yako sio siku na usiku huu, bali makusudio yako ilikuwa ni kutengana nae na kumtaliki, basi Talaka itakuwa imepita ambayo ulikusudia. Nayo ni Talaka moja, haikupita isipokuwa Talaka moja tu. Ikiwa mwanzoni alikuwa hajamtaliki Talaka mbili, anaweza kumrejea maadamu bado angali ndani ya eda. Hali hii ni kama alikusudia Talaka. Ama ikiwa makusudio yake ilikuwa ni kumkataza siku hiyo tu, kutakuwa hakukupita kitu. Swali: 38 Mimi ni mwanaume ambaye nimeoa na nina matangamano na mke wangu mazuri sana kwa daraja ambayo nilimwambia "uso kukutana na wangu ni Haramu ukinificha kitu kinachohusiana na maisha yetu ya kindoa." Lakini nimekuja kuona kuwa jambo hili ni khatari, na nataka kuelekezwa katika jambo ambalo litanitoa katika sharti hii. Ipi hukumu ikiwa mke wangu atanificha kitu bila ya mimi kujua? Imaam Ibn Baaz: Ikiwa makusudio ni kumkataza asikufiche chochote, inatosha kwako kutoa kafara ya yamini. Na wala sio lazima kwake kukubainishia kila kitu, ikiwa ni mambo yaliyopita. Akubainishie mambo yenye faida. Ama yanayoweza kumdhuru katika mambo ambayo ni maslahi maalumu yanayomuhusu yeye au yakakudhuru wewe, sio lazima kwake kukubainishia. Lakini akubainishie yanayohusiana na maslahi yako na maslahi ya nyumba yako. Na ikiwa unataka kujitoa katika hilo ni juu yako kutoa kafara ya yamini, ni juu yako kutoa kafara ya yamini na inatosha. Kwa kuwa makusudio yako (kusema hivyo) ni kumhimiza kukubainishia kila kitu na wala asikufiche kitu. Ukitoa kafara ya yamini inatosha. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Kama utakula yamini ukaona lingine ni bora kuliko hilo basi lifanye hilo bora na fanya kafara la yamini yako.” Na hii hukumu yake ni kama ya yamini. Ni juu yako kuleta Tawbah juu ya hilo, kwa kuwa kuharamisha ni jambo lisilojuzu. Ni juu yako kutubu kwa Allaah (Ta´ala) na utapotoa kafara ya yamini yako hakuna neno. Muhimu ni wewe utoe kafara kwa yamini yako. Muulizaji: Hata kama kwa kusema kwake huko amekusudia (mke huyo) kuharamika kwake? Imaam Ibn Baaz: 39 Ikiwa amekusudia kuharamika kwake, huyu ni juu yake kutoa kafara ya Dhwihaar. Ama ikiwa amekusudia kumhimiza (kufanya au kutofanya kitu)... Na hii ndio dhahiri (ya makusudio ya muulizaji). Watu wengi kwa mfano wa hili, wanakuwa wanakusudia kuhimiza ili kumtisha (mke wake). Kwa hali hii atatoa kafara ya yamini. Ama ikiwa ndani ya moyo wake amekusudia kuharamika kikamiifu, hii itakuwa ni Dhwihaar na ni juu yake kutoa kafara ya Dhwihaar. Nayo ni kuacha mtumwa huru, asiyeweza afunge miezi miwili mfululizo na asiyeweza alishe masikini sitini kwa chakula kimechozoelekea mjini; kila masikini atampa 1,5 kg kabla ya kumgusa (kumjamii). Ikiwa alikusudia hili - kuharamika - naye akathibitisha kuwa amemficha kitu, atatoa kafara hii na yatosha. Ama akithibitisha ya kuwa hakumficha kitu, hana juu yake kitu. Muulizaji: Vipi ikiwa atamficha na asimwambie hilo? Imaam Ibn Baaz: Ikiwa anajua kihakika ya kuwa kamficha kitu, ni juu yake kutoa kafara... Muulizaji: Lakini nakusudia ikiwa (mke) amemficha kitu wala yeye (mume) hakujua kitu... Imaam Ibn Baaz: Hana juu (mume) kitu. Lakini akimweleza, ni juu yake atoe kafara. Swali: 40 Nimemtaliki mke wangu na kumwambia: "Ukimuomba mwanaume kukuoa, olewa" na nikampa karatasi yake (ya Talaka). Je, naweza kumrudi mara ya pili? Imaam Ibn Baaz: Talaka ikiwa ni kwa matamshi kama haya, inakuwa imepita mara moja. Akimwambia: "Ukikubaliana na mwanaume mwengine waweza kuolewa", "mwanaume mwengine akikichumbia, olewa" au mfano wa matamshi kama hayo, au "wewe nimekutaliki", au "wewe umetalikika" au mfano wa hayo, hii huchukuliwa ni Talaka moja tu. Anaweza kumrudi maadamu bado angali ndani ya eda, kwa kushahidisha mashahidi wawili ya kwamba kamrejea mke wake. Bora zaidi, awashuhudishe mashahidi wawili ambao ni waadilifu, washuhudie ya kuwa kamrudi mke wake maadamu bado angali ndani ya eda, yaani maadamu katwaharika hedhi mara tatu ikiwa ni mwanamke mwenye kupata hedhi. Na ikiwa ni mwanamke ambaye hapati hedhi, eda yake ni miezi mitatu. Akimrudi ndani ya miezi hii mitatu, mwanamke huyo anakuwa ni Halali kuwa mke wake. Ama ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi, eda yake (inaisha) kwa kupata hedhi tatu, ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi. Na ikiwa ni mzee na hapati hedhi, eda yake ni miezi mitatu. Ama ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi, eda yake (inaisha) kwa kupata hedhi tatu, ikiwa ni mwanamke wa kupata hedhi. Na ikiwa ni mzee na hapati hedhi na binti mdogo (ambaye hajaanza kupata hedhi), eda yake ni miezi mitatu. Ikiwa hakumuwahi ndani ya muda wake huyo wa eda, basi mwanamke huyo atakuwa ni ajinabi kwake. Hatokuwa Halali kwake isipokuwa kwa ndoa nyingine mpya kama wanawake wengine ambao anaweza kuwachumbia. Hawi Halali isipokuwa kwa kufunga ndoa mpya na masharti yanayokubalika Kishari´ah. Swali: 41 Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah inajuzu? Kwa kuwa huku kwetu watu wanamchinjia mtu ambaye anaitwa "Mujalliy". Na tunapowauliza ni nani Mujalliy? Wanasema kuwa ni Nabii katika Manabii wa Allaah. Tunaomba utupe faida. Imaam Ibn Baaz: Kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah ni munkari mkubwa na ni Shirki kubwa, sawa ikiwa kachinjiwa Nabii, walii, nyota, jini, sanamu au visivyokuwa hivyo. Kwa kuwa Allaah (Subhaanah) Anasema: ْ ل ْ ِّرب َٰب َ ِين ُو َص ُ ِْك أُمِر َ ل ْ ُق ُ و ُ َيك ل ُ ن ِين َّ َوأَ َنا أ ِ ماتِي لِلَّـ َ المُسْ لِم َ ت َ ذل َ ۚه َ ر َ عالَم َ ال َ ه َم َو َ اي َ محْ َي َو َ سكِي َ َلتِي َ َّل إِن ِو ِش "Sema (ee Muhammad )صلى هللا عليه وآله وسلم: “Hakika Swalaah yangu, na Nusukiy (kuchinja kafaara na ‘ibaadah zangu) na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah (Pekee) Mola wa walimwengu. Hana mshirika, na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni Muislamu wa kwanza (waliojisilimisha kwa Allaah).” (06:162-163) Akaelezea (Subhaanah) kuwa kuchinjiwa ni kwa ajili Yake kama Swalah ilivyo Yake. Atakayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, ni kama aliyeswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Atakuwa kamshirikisha Allaah (´Azza wa Jalla). Hali kadhalika Anasema (Subhaanah): ْ اك َ ْنا أَع َّ ِإ َ ر َ ال ْحر ِّ ص َ وا ْن َ ِّك َ ِرب َ لل َ ف َ ك ْو َث َ ط ْي َن "Hakika Sisi Tumekupa (ee Muhammad )صلى هللا عليه وآله وسلمAl-Kawthar (mto katika Jannah). Basi swali kwa ajili ya Mola wako na chinja (kwa ajili Yake)." (108:01-02) Swalah na kuchinja ni ´Ibaadah mbili muhimu sana. Atakayewachinjia walio ndani ya makaburi, Manabii, nyota, sanamu, jini au Malaika, basi atakuwa amemshirikisha Allaah. Ni kama mfano wa kuswali kwa ajili yao, au kuwataka msaada (kwa wasiyoyaweza) au kuwawekea nadhiri, yote haya ni kumshirikisha Yeye (Subhaanah). Na Allaah (Subhaanah) Anasema: ْ َّوأَن َف َ ه ًح ْ َل َت دا ِ ع اللَّـ ِ جدَ لِلَّـ َ َه أ َم َ دعُوا َ م َ ال َ ِ سا "Na kwamba Misikiti ni (kwa ajili) ya Allaah, basi msiombe (msimuabudu) yeyote pamoja na Allaah." (72:18) 42 Na Anasema (Subhaanah): ْ ت َّ ِنس إ ْ َخل ُ ق َ ما ُب ُ ْل ِل َيع ون َ اْل َ َّجن َو َ ِ ال ِ د ِْ و "Na Sikuumba majini na watu wa isipokuwa waniabudu." (51:56) Na Anasema (Subhaanah): ْ ب َّ ِدوا إ َّ َُّك أ ٰض َو ُب ُ ل إِيَّا ُ ْل َتع سا ًنا َ ْْن إِح َ ال َ ه َ رب َ ى َ ق َ ِ والِدَ ي ِو "Na Mola wako Amehukumu kwamba: “Msiabudu (yeyote) isipokuwa Yeye Pekee na (Ameamrisha) kuwafanyia wema wazazi wawili." (17:23) ´Ibaadah ni haki ya Allaah Pekee; na kuchinja ni miongoni mwa ´Ibaadah, kutaka msaada ni katika ´Ibaadah na Swalah ni katika ´Ibaadah. Na imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema: "Allaah Amlaani mwenye kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah." (Swahiyh Muslim, Hadiyth kutoka kwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anhu)) Ni juu yenu kuwakataza watu hawa na kuwafunza ya kwamba hii ni Shirki kubwa na kwamba lililo la wajibu juu yao ni kuacha hilo. Hawafai kwao kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama ambavyo hawafai kuswali kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Na hili, ni kwa ajili ya kusaidia katika wema na uchaji Allaah, kukataza maovu, na kulingania katika Dini ya Allaah na kumpwekesha Allaah kwa kumtakasia ´Ibaadah Yake. Kwa minajili ya Tawhiyd. Ni wajibu ´Ibaadah iwe kwa Allaah Mmoja (Subhaanahu wa Ta´ala). Ni wajibu kwa wanachuoni, wanafunzi na Waislamu kusaidiana juu ya wema na uchaji Allaah na wakataze Shirki kwa yule mwenye kuifanya, mpaka iweze kudhihiri Tawhiyd na kushikwe vikwazo kwa sababu zinazopelekea katika Shirki. Swali: Ni yapi maoni yako kufuatilia kisimo cha Qur-aan Tukufu katika idhaa ya Qur-aan na kusoma pamoja naye na mimi huku niko nafanya kazi? 43 Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya kufuatilia Qur-aan, lakini iwe kwa kunyamaza na isiwe kwa kusoma. Allaah (Subhaanah) Anasema: ْ ئ َ ِوإ ُ م ُ َّعل ُ ِوأَنص َ ُالقُرْ آن ُ َمعُوا ل ُون ِ فاسْ َت َ حم َ ْتر َ َتوا ل َ ه َ ر َ ْك ِ ُذا ق "Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya (mzingatie) mpate kurehemewa." (07:204) Wewe sikiliza na uzingatie anayosoma msomaji na ustafidi kwayo. Ama kusoma pamoja naye hapana. Sunnah ni kunyama, kuzingatia maana yake na kusikiliza mpaka uweze kustafidi kwa Maneno ya Mola Wako (´Azza wa Jalla). Lakini usisome pamoja na msomaji, nyamaza. Hii ndio Mashru´ah. Swali: Nikiwa katika safari ambayo mtu anaweza kufupisha Swalah, na Swalah ya ´Aswr ikanifikia na sikuiswali mpaka wakati wake ulipokwisha na nikafika kwa ahli zangu. Je, nilipe Swalah ile kwa kufupisha au kikamilifu? Imaam Ibn Baaz: Msafiri akifika kwa ahli zake, analipa (Swalah) zilizompita kikamilifu na hafupishi. Anafupisha tu katika hali yake ya safari, ama akichelewesha kwa mfano ´Aswr, au Dhuhr au ´Ishaa mpaka akafika kwa ahli zake, ataswali Rakaa´ nne, kwa kuwa rukhusa alikuwa nayo katika hali ya safari. Swali: Ikiwa mtu ametawadha au yuko katika Wudhuu, akamgusa mama yake au dada yake. Je, Wudhuu wake unavunjika? 44 Imaam Ibn Baaz: Kauli sahihi ni kwamba, kumgusa mwanamke hakuvunji Wudhuu, sawa ikiwa ni mke wake au wanawake wengine. Hii ndio kauli sahihi. Na kuna tofauti kwa wanachuoni. Wanachuoni kuhusiana na hili wana kauli tatu: 1) kumgusa mwanamke kunavunja Wudhuu kabisa, 2) hakuvunji Wudhuu kabisa na 3) kuna ufafanuzi, kunavunja Wudhuu ikiwa amemgusa kwa matamanio, vinginevyo hapana. Na kauli yenye nguvu katika kauli hizi tatu ni kwamba, (kumgusa mwanamke) hakuvunji Wudhuu kabisa. Kutokana na yaliyothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa aliwabusu baadhi ya wake zake kisha akaswali na wala hakutawadha. Na ni kwa sababu, asli ni kuwa mtu anabaki na Twahara na wala haivunjiki isipokuwa kwa kitu cha wazi. Na ni kwa sababu jambo hili wanakumbana nalo sana katika manyumba yao, na lau kumgusa mwanamke kungekuwa kunavunja Wudhuu angelibainisha hilo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ubainisho wa wazi na asingelificha. Ama Kauli Yake (´Azza wa Jalla): ِّ م ال ُ ْمس َ أَ ْو ء َ سا َ ن َل ُت "Au mmewagusa (mmewaingilia) wanawake." (04:43) Makusudio ya hilo ni Zinaa, kama alivyosema hilo Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na wengineo. Makusudio ni jimaa, Allaah Kaiita kwa jina na kugusa. Allaah Kaipa jimaa kunya kwa lafdhi kama hii na kwa "kukutana". Hii ndio kauli sahihi, ya kuwa kumgusa mwanamke hakuvunji Wudhuu isipokuwa tu mtu akitokwa na kitu, kama madhiy. Vinginevyo hakutengui Wudhuu. Swali: Huku kwetu watu wanawasomea Qur-aan maiti na wanachukua ujira kwa hilo. Anapokufa mmoja wao wanamsomea Qur-aan kwa siku tatu, wanamchinjia na kumfanyia walima. Je, maiti wanafaidika kwa lolote na je hili ni katika Shari´ah? 45 Imaam Ibn Baaz: Hili ni Bid´ah. Kumsomea maiti na kuchukua ujira kwa hilo, hili ni Bid´ah na wala halijuzu. Hakuna cha ujria na wala haifai kwake kumsomea maiti na wala hakuna dalili ioneshayo kuwa atanufaika kwayo, bali hili ni munkari na Bid´ah. Hali kadhalika, kumchinjia na kumfanyia chakula, yote haya ni Bid´ah na munkari na hayajuzu. Ni wajibu kutahadhari hilo na kuwatahadharisha watu kwa hilo. Hili ndilo la wajibu kwa wanachuoni na kwa watawala. Wawatanabahishe watu kwa Aliyokataza Allaah, na wawachukulie hatua wajinga na wapumbavu mpaka waweze kunyooka katika njia iliyonyooka ambayo Allaah Kawawekea nayo waja Wake. Kwa hilo, hali na jamii itatengemaa, na itadhihiri hukumu ya Kiislamu na mambo ya Kijaahiliyyah yataisha. Swali: Mwanaume wa Kiislamu akimtukana mke wake au Dini yake anakuwa ni mwenye kutalikika Kishari´ah kama tunavyosikia kwa watu wengi? Imaam Ibn Baaz: Akimtukana mke wake hatalikiki. Lakini ni juu yake atubu kwa Allaah na apatane na mke wake. Na ikiwa watasameheana, hakuna kitu. Na ikiwa atamtusi kama (mke) alivyomtusi kwa kulipiza kisasi bila ya kuzidisha juu ya hilo, haina neno. Na ikiwa atamsamehe ndio bora zaidi. Kwa kuwa Allaah Anasema: ْت ْ َُو أ َّ ربُ لِل ٰو ى َق َق َ اعْ دِلُوا ه "Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa." (05:08) Ama kumtukania Dini yake ilihali naye (mwanamke huyo) ni Muislamu, huu ni ukafiri. Tunamuomba Allaah afya. Ikiwa mume ni Muislamu na mke ni Muislamu, kutukana Dini yake ina maana kautukana Uislamu. (Mke) asiishi naye (huyo mume). Atiwe adabu (huyo mume) na apigwe kwa kitendo chake 46 hichi kibaya na aambiwe kutubia.Akitubu kwa kitendo chake hichi kibaya (ni vizuri) la sivyo ni wajibu (mume huyo) kuuawa. Ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu au kiongozi wa nchi wamfanye atubu, la sivyo auawe. Kwa kuwa kutukana Dini ya Kiislamu ni katika aina mbaya kabisa za ukafiri zinazovunja Uislamu (wa mtu). Hali kadhalika kumtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kutukana Qur-aan. Swali: Je, kukata kucha baada ya Wudhuu na kunyoa ndevu kunavunja Wudhuu au hapana? Imaam Ibn Baaz: Kukata kucha hakutengui Wudhuu, hali kadhalika kunyoa ndevu na kichwa. Kunyoa kichwa hakuvunji Wudhuu na wala sio katika mambo yanayovunja Wudhuu. Lakini kunyoa wala kupunguza ndevu haijuzu. Kwa kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema: "Punguze masharubu na zirefusheni ndevu, mjitofautishe na washirikina." Na anasema (´alayhis-Swalaat was-Salaam): "Punguzeni masharubu na zirefusheni ndevu mjitofautishe na Majuus (waabudu Moto)." Kasema: "... zirefusheni ndevu." Kaamrisha (´alayhis-Swalaat was-Salaam) kuzirefusha, kuzifanya kuwa ndefu na kuzifuga. Haijuzu kwa Muislamu kuzinyoa wala kuzipunguza, kamwe. Badala yake, ni wajibu kuzirefusha, kuzifanya kuwa ndefu na kuzifuga. Kwa kuwa, katika kufanya hivyo kuna kwenda kinyume na washirikina na kushikamana na mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kuna kujitofautisha na wanawake. 47 Swali: Akitawadha mtu kwa ajili ya Swalah, na njiani akakutana na mnaswara au myahudi na wakapeana mikono. Je, Wudhuu wake unatenguka? Na ipi hukumu kuwaalika manaswara kula chakula katika nyumba ya Muislamu? Imaam Ibn Baaz: Akipeana mikono na manaswara au mayahudi na makafiri wengine atakaokutana nao, Wudhuu hautenguki. Atabaki na Twahara yake. Lakini haifai kwake kupeana nao mikono wala kuanza yeye kuwaongelesha. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Msianze kuwapa mayahudi wala manaswara Salaam." Na kupeana mikono ni baya zaidi. Tusemeje kupeana nao mikono? Asianze kuwapa Salaam wala kupeana nao mikono. Lakini, wao wakianza kutoa Salaam na kukupa mkono, hakuna ubaya kumjibu. Ama yeye kuanza, hapana asianze. Ama kuwaalika katika walima na kula chakula, hili linahitajia ufafanuzi. Ikiwa malengo ni kutaka kumkaribisha katika Uislamu, kumpa nasaha na kumlingania katika Uislamu, hili halina neno. Ama kumualika katika chakula kwa ajili ya Swadaqah na urafiki, hapana. Kwa kuwa baina yetu sisi (Waislamu) na wao kuna uadui na chuki. Swali: Je, inajuzu kusoma kwa sauti katika Swalah za kusomwa kwa siri? Imaam Ibn Baaz: Kujuzu inajuzu, lakini kusoma kwa siri ni bora. Wakati fulani alikuwa akisoma kwa sauti, anasoma kwa sauti Aayah. Lakini mara nyingi, alikuwa 48 akisoma kwa siri (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Hii ndio Sunnah. Alikuwa akisoma kwa siri kama katika Swalah ya Dhuhr na ´Aswr, lakini kusoma kwa sauti katika baadhi ya nyakati, hivi ndio bora. Swali: Je, inajuzu kusoma Qur-aan sokoni katika wakati ambapo ninakuwa sina kazi? Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya kusoma Qur-aan katika duka lako au mahali pa kazi kwako, ukiwa na uwezo wa hilo utasoma utachoweza katika Kitabu cha Allaah, au utamdhukuru Allaah au utamswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Unapokuwa huna kazi, jishughulishe na kumdhukuru Allaah (´Azza wa Jalla); kwa kusoma Qur-aan, kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kwa kusoma vitabu vyenye faida. Mambo yote haya ni mazuri. Swali: Sisi katika mji wetu ikiwa mtu anaitakidiwa kuwa ni mwema, basi wanamfanya mtoto wake kuwa Khalifah baada yake. Na akifa mtoto huyu, wanaweka Khalifah mwingine badala yake kutoka katika watoto wake, hali inaendelea hivi wanarithiana Ukhalifah. Na wote hawa, (watu) wanaamini kuwa ni wema na wana baraka, na watu wanabusu mikono yao. Na wanawaletea mali na kuwawekea nadhiri kwa kuomba baraka. Ipi hukumu ya Kishari´ah kwa hilo? Imaam Ibn Baaz: 49 Haya ni katika matendo ya baadhi ya Suufiyyah. Na hili ni jambo lisilokuwa na asli katika Shari´ah. Bali haya ni katika mambo ya ukhurafi ambayo yamezushwa na baadhi ya watu wa Ahl-ul-Taswawwuf kurithiana Ukhalifah. Haya hayana asli. Na baraka kuchukuliwa kutoka kwa baadhi ya watu, hili halina asli na ni jambo lisilojuzu. Bali hili ni katika maovu na njia inayopelekea katika Shirki kubwa. Baraka zinatoka kwa Allaah (Ta´ala). Yeye ndiye Huleta baraka (Subaanahu wa Ta´ala). Na wala baraka haitafutwi kutoka kwa asiyekuwa Yeye. Kuitafuta kutoka kwa Zayd au ´Amr akupe baraka, hili ni jambo lisilokuwa na asli. Bali ni katika Shirki, ikiwa utamuomba nayo na ukaamini kuwa anawabariki watu na mwenye kuleta baraka ni yeye, hii ni katika Shirki kubwa. A´udhubi Allaah. Ama akidhani (mwenye kufanya hivyo) kuwa, kumtumikia au kumtii kuna baraka kwa kuwa ni katika watu wema na anataraji kwa hili kupata thawabu akimtii au kumsaidia kwa kitu, hili yategemea. Ikiwa huyu mwenye kutiiwa ni mwanachuoni katika wanachuoni wa Waislamu au ni katika watu wema wanaomuabudu Allaah ambao wanajulikana ni wenye misimamo na anamtii Allaah na Mtume Wake, akamsaidia kwa ajili ya Allaah, akamtatulia haja yake na akamtembelea kwa ajili ya Allaah na si kwa ajili ya kutafuta baraka kutoka kwake, au akamtembelea mgonjwa, haya ndio maadili ya Waislamu na ni jambo limependekezwa. Kwa minajili ya kutembeleana, kumtembelea mgonjwa, kumtembelea ndugu yako kwa ajili ya Allaah, hili ni haki. Ama (kumtembelea) kwa minajili ya kumuomba baraka, hili ni jambo lisilojuzu. Kwa kuwa hili halina asli yoyote, isipokuwa hili ni kwa haki ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) peke yake. Allaah Kamfanya kuwa ni mwenye baraka. Hakuna ubaya mtu akakusudia kutafuta baraka kutoka katika maji yake, nywele zake n.k., yeye ana baraka (´alayhi-Swalaat wasSalaam). Na hili la kutabaruku kwake lilikuwa linafanywa na Maswahabah. Hili ni jambo ambalo ni maalumu kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na si kwa mwingine yeyote. Ni wajibu kwa Waislamu wajue hili, na wajiepushe na ukhurafi huu ambao unafanywa na Suufiyyah, Tijaaniyyah na Shaadhiliyyah na Ukhalifa huu ambao wanarithiana, halina asli na ni jambo la batili. Ni jambo ovu na njia inayopelekea katika Shirki. A´udhubi Allaah. 50 Swali: Je, inatosha kusema "Bismillaah" bila ya kuelekea Qiblah, au ni lazima kufanya yote mawili (kusema Bismillaah na kuelekea Qiblah)? Kwa kuwa mahala ambapo nafanya kazi ni pafinyu na wala siwezi kuelekea Qiblah wakati wa kuchinja. Imaam Ibn Baaz: Kusema "Bismillaah" wakati wa kuchinja ni jambo la wajibu, kwa kuwa Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kaamrisha hilo, na namna hii ndivyo alivyoamrisah Mtume (´alayhis-Swalaat was-Salaam). Haijuzu mtu kukusudia kuacha kusema "Bismillaah". Mtu anatakiwa kusema wakati wa kuchinja "Bismillaah Allaahu Akbar". Hii ndio Sunnah. Na lau atasema "Bismillaah" yatosha. Haifai kwake kukusudia kuacha kusema "Bismillaah". Akiiacha kwa kusahau au kwa ujinga wa kutokujua, hakuna neno kwa hilo na kichinjo kitakuwa ni Halali. Lakini haifai kwake kuiacha kwa kukusudia. Ama kuelekea Qiblah ni jambo limependekezwa na wala sio lawajibu. Lau atachinja bila ya kuelekea Qiblah, ni sahihi na inajuzu. Lakini kuelekea kwake Qiblah wakati wa kuchinja ndio bora. Swali: Baadhi ya maamuma wakitoa Salaam moja upande wa kulia kabla ya Imamu kwa kusahau. Je, Swalah zao zinabatilika? Imaam Ibn Baaz: Swalah yake haibatiliki. Lakini itabidi watoe Salaam baada yake mara mbili. Swali: 51 Ni yapi mahari ya Kishari´ah kwa msichana ambaye hajaolewa na mwanamke ambaye kishatalikiwa? Imaam Ibn Baaz: Mahari hayana mpaka maalumu. Hakukutengwa mahari maalumu kwa yule ambaye hajaolewa, ambaye katalikiwa wala yule ambaye kafiwa. Atayowekea hata kama yatakuwa ni madogo, yatosha. Sawa mwanamke huyo alikuwa ni bikira hajaolewa, alikuwa amekatalikiwa au alikuwa amefiwa. Watayopatana mwanaume na mwanamke yanatosha, sawa yakiwa madogo au yakiwa mengi. Swali: Baada ya kukoga janaba, natokwa na kitu kama manii. Je, ni wajibu kwangu kurudi kukoga tena? Imaam Ibn Baaz: Hapana sio wajibu, maadamu umekwishakoga manii haya hayana maana yoyote. Kwa kuwa yametoka bila ya shahawa, hukumu yake ni kama ya mkojo, hayana maana yoyote. La wajibu ambalo ni kukoga umekwishatekeleza, haidhuru kutoka kwa manii ambayo ni athari ya jimaa uliofanya. Hali kadhalika mwanaume, lau atakoga kisha yakamtoka baada ya hapo pamoja na mkojo, haidhuru hilo maadamu alikoga kwa jimaa aliofanya mwanzoni. Ama yakitoka kwa shahawa nyingi, au kwa kupapa sana, au kwa kubusu au kwa mfano wa hayo katika mambo ambayo ni sababu ya kutoka kwa manii kwa shahawa, haya yatakuwa ni manii mapya ambayo yanahitajia kukoga. Ikiwa yametoka kwa shahawa mpya; sawa ikiwa ni kwa kuangalia, kupapasa au kubusu, haya hukumu yake itakuwa ya janaba mpya. Ni juu ya yule ambaye yamemtoka akoge upya sawa ikiwa ni mwanaume au mwanamke. Ama ikiwa ni (athari ya) yaliyobaki kwa (kitendo) alichokifanya nyuma, hayadhuru na wala hayahitajii kukoga upya. 52 Wanaosema Kuwa Qur-aan Imeumbwa Na Kutoonekana Allaah Qiyaamah Swali: Ipi hukumu kwa mwenye kujinasibisha na madhehebu ambayo yanaamini kuwa Qur-aan imeumbwa, na kwamba watu hawatomuona Allaah siku ya Qiyaamah, kwa kuzingatia ya kwamba yule anayejinasibisha na madhehebu haya mara nyingi hawakiri kuumbwa kwa Qur-aan wala hawaamini hivyo [wao] na wanasema sisi hatuamini kuwa Qur-aan imeumbwa, lakini sisi tunajinasibisha na madhehebu haya kwa kuwa baba zetu walikuwa wakijinasibisha kwayo tu. Na je, ipi hukumu ya mwenye kuamini kuwa Quraan imeumbwa? Je, anachukuliwa katoka katika Uislamu? Imaam Ibn Baaz: Ndio, mwenye kuamini kuwa Qur-aan imeumbwa ina maana anapinga kuwa sio Maneno ya Allaah. Hii ni Shirki kubwa. Hukumu hii hali kadhalika kwa yule mwenye kupinga kuonekana kwa Allaah siku ya Qiyaamah Peponi. Hii ni Shirki kubwa. Kwa kuwa amemkadhibisha Allaah na amemkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo kila kikundi au mtu asemae Qur-aan imeumbwa, ina maana [anapinga] si Maneno ya Allaah. Bali anaona ni maneno ya kiumbe yameumbwa atamka nayo. Na Allaah Kasema kuwa ni Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na Allaah Kasema kuwa ni Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Katika Kauli Yake: ْ ِّن ْ م َّ ح َ ع َ ك ٌح ُ ال هللا ِّ م َم َ ْتى َيس َ ُجرْ ه َ ار َ ج َ ِين اسْ َت َ رك َ دم َ َوإِنْ أ َ َ َكَل ِ َ فأ ِش "Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia Maneno ya Allaah." (09:06) Kasema tena Allaah (Ta´ala): َك َ دلُوا ِّ ي َب ُ ُري ُ ون أَن هللا ِ َّ م َ د َ َل ِي "Wanataka kuyabadili Maneno ya Allaah.” (48:15) 53 Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwaambia watu: "Aletwe kwanza mpaka afikishiwe Maneno ya Allaah." Ilikuwa ni wakati bado wanasubiri kufanya Hijrah kutoka Makkah, akaawambia: "Wasimhame kwanza mpaka afikishiwe Maneno ya Allaah." Makusudio ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wote walikubaliana kuwa Qur-aan ni Maneno ya Allaah. Na Qur-aan yenyewe inaonesha dalili kuwa ni Maneno ya Allaah. Atakayedai kuwa Qur-aan imeumbwa basi amedai kuwa sio Maneno ya Allaah. Anakufuru kwa hili. Kwa kuwa kamkadhibisha Allaah na Mtume Wake na Ijmaa´ [makubaliono ya Maswahabah] ya Waislamu. Hali kadhalika kwa mwenye kupinga Sifa za Allaah na akapinga kuonekana. Mwenye kusema [Allaah] sio Al-Haliym, Al-Hakiym, Al-´Aziyz, Al-Qadiyr na Sifa Zake zingine. Huyu ni kafiri kama Jahmiyyah. Hali kadhalika mwenye kupinga kuonekana kwa Allaah, kuwa hatoonekana Aakhirah wala Peponi. Huyu ni kafiri kufuru kubwa. A´udhubi Allaah. Tunamuomba Allaah afya. Kwa kuwa kamkadhibisha Allaah na Mtume Wake. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Kasema kwa haki ya makafiri: َّ ك َّ َِل إ َ ُن ُون َ محْ جُ وب َ َّمئِذ ل َ م َي ْو َ م ْ ِّه ْه ِ عن رَّ ب "Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa kumuona Mola Wao." (83:15) Asiyemuitikia Allaah [katika hili] ni kafiri, ina maana waumini watamuona Mola Wao (Subhaanahu wa Ta´ala). َّ مئِذ ٌرة ِّ ر َ ِها َناظ َب َ رةٌ إِلَى َ ِناض َ وُ جُوهٌ َي ْو "Zipo nyuso siku hiyo zitaong'ara, zinamwangalia Mola Wao." (75:22-23) "Kungara" kutokana na Uzuri Wake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Na Kasema tena Allaah (Jalla wa ´Alaa): ْ نو ْا ُس ٌ َز َياد ة َ الحُسْ َنى َ ِْين أَح َ لِّلَّذ ِو "Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi." (10:26) 54 Maana ya "Ziada" katika Hadiyth sahihi kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Husna [wema] ni Pepo, na ziada ni kuangalia Uso wa Allaah." Na imekuja katika Hadiyth Swahiyh Mutawaatir kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amesema: "Hakika nyinyi mtamuona Mola Wenu kama mnavyouona mwezi mpevu. Hakuna kitu kitakachowazuia kumuona siku hiyo." Na akasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika upokezi mwingine: "Kama mnavyouona mwezi mpevu. Na kama mnavyouona mwezi usiku wa al-Badr. Na hakuna kitu kitakachowazuia kumuona siku hiyo." Ina maana kuonekana kwa Allaah ni jambo la wazi kabisa, ni kitu hakina utata wala shaka. Makusudio ni kuwa waumini siku ya Qiyaamah watamuona Mola Wao waziwazi kama uonekanavyo mwezi wazi kabisa bila ya pazia. Hali kadhalika Peponi watamuona Mola wao (Jalla wa ´Alaa). Atakayepinga hili na kusema hatoonekana kamkadhibisha Allaah na Mtume Wake hivyo anakuwa kafiri. Tunamuomba Allaah afya. Chanzo: http://www.binbaz.org.sa/mat/10243 Swali: Kuna mtu katika mji wetu hafungi wala haswali. Na nimemuona kwa macho yangu anacheza kamari. Na watu wake wanadai kuwa ni katika mawalii na watu walio karibu ya Allaah. Na kuna watu waaminifu wamenieleza ya kuwa anamtukana Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati nilipomkataza kitendo hichi kichafu, wakadai watu wake ya kuwa hii ni hali yake kwa uinje, ama kwa udani ni muumini. Ipi hukumu ya Kishari´ah kwa mfano wa huyu? 55 Imaam Ibn Baaz: Huyu ni mnafiki na wala sio muumini. Mfano wa watu kama hawa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Mawalii wa Allaah ni wale wenye Imani na Taqwa. Anasema Allaah (Subhaanah): ُ كا ُم ُز َو َ ه َ َأ َو َ ْم َيح َ ل ُ ل ون ِ ء اللَّـ َ ُنوا َي َّتق َ نوا َ ِين آ َ ون الَّذ َ ن َ م َ ٌخ ْوف َ ل إِنَّ أَ ْولِ َيا ْه ْ ْه ِ ع َلي "Tanabahi! Hakika awliyaa wa Allaah (vipenzi Vyake wanaoamini Tawhiyd ya Allaah na kufuata amri Zake) hawana khofu juu yao, na wala hawatohuzunika. Wale walioamini na wakawa wana taqwa (wanafuata amri za Allaah na Mtume Wake Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” (06-26:01( Namna hii ndivyo ilivyo katika Suurat Yuunus, hizi ndizo sifa za mawalii wa Allaah; ni wenye Imani na Taqwa kwa nje na kwa ndani. Na Akasema tena (´Azza wa Jalla): ْ ل َّ ِه إ ْ َو َل ٰـكِنَّ أ َ م ُ كا َّ م ۚ ُءه َ ما ُر ُ ال ُ ُۚ إِنْ أَ ْولِ َياؤ ُون َ ل َيعْ لَم َ ك َث َ ون َ ُتق َ نوا أَ ْولِ َيا َو َ ْه "Na hawakuwa walinzi (awliyaa) wake (Msikiti huo). Hawakuwa walinzi (awliyaa)wake isipokuwa wenye taqwa; lakini wengi wao hawajui." (08:34) Anasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Watu wa (... sauti haiko wazi... ) sio katika mawalii wangu, isipokuwa mawalii wangu ni waumini." Mawalii wa Allaah na mawalii wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni waumini na watu wa Taqwa. Yule mwenye kujidhihirisha kwa kuacha Swalah, Swawm na anamtukana Allaah na Mtume Wake, huyu sio katika mawalii wa Allaah, bali ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na ni wajibu aambiwe kutubu vinginevyo auawe, ni wajibu kwa mtawala wa Waislamu amwambie atubie la sivyo auawe. Kwa kuwa mwenye kuacha Swalah ni kafiri, aambiwe kutubu la sivyo auawe. Na mwenye kumtukana Allaah na Mtume wake, huyu anauawa hata bila ya kuambiwa kutubia kutokana na wanavyoona kundi katika wanachuoni. Muhimu ni kuwa, mtu huyu na watu mfano wake sio katika mawalii wa Allaah, isipokuwa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na wale wanaomtetea na kumhami na kusema kuwa kwa nje ni namna hii tu, lakini kwa ndani ni 56 muumini, watu hawa ni katika jinsia yake nao ni mawalii wa Shaytwaan. Na ni watetezi wa shari na ufisadi. Baadhi ya Suufiyyah waliodanganywa ndio hufanya hivi. Ni wajibu kutanabahi kwa hili. Wanachuoni wa Sunnah (Rahimahumu Allaah) wamesema kwa yule mwenye kudai ni walii: "Lau atatembea angani, akatembea juu ya maji, hazingatiwi kuwa ni katika mawalii wa Allaah mpaka matendo yake yatazamwe kwanza na kupimwa kwa mizani ya Kishari´ah.” Akisimama katika mipaka ya Kishari´ah na kujulikana kuwa ni mwenye msimamo juu ya utiifu wa Allaah na Mtume Wake na kujiweka mbali na maharamisho ya Allaah na Mtume Wake, huyu ndiye muumini na walii. Na yakionekana kwake mambo ya ufasiki, kufanya ya haramu au kuacha ya wajibu, haya ni dalili tosha kuwa ni katika mawalii wa Shaytwaan na sio katika mawalii wa Allaah." Kama alivyosema haya Imaam Shaafi´iy na Ahmad (Rahimahuma Allaah) na wasiokuwa wao katika wanachuoni. Muhimu ni kuwa, mfano wa watu kama hawa ni katika mawalii wa Shaytwaan. Na ni wajibu kwa mwenye kujua hilo kupeleka suala lake kwa kiongozi wa Waislamu mpaka ampe kinachomstahiki; amwambie kitubu la sivyo amuue. Swali: Kulitokea baina yangu mimi na mke wangu tofauti kisha siku hiyo nikampiga kutokana na ghadhabu niliokuwa nayo, akalia na kunambia "nataka unitaliki". Nikamwambia "vaa nguo zako nikupeleke kwa familia yako". Alipokuwa anataka kuvaa nguo zake nikawa nimemkataza kufanya hivyo na tukapatana siku hiyo hiyo kama kwamba hakukupitika kitu. Na hapo ilikuwa miezi miwili iliopita. Lakini nafsi yangu inanambia mara kwa mara mbali na muda wote huu kuhusu hukumu ya Kishari´ah kutokana na tulioambizana. Na je, kwa hayo Talaka itakuwa imepita? Imaam Ibn Baaz: 57 Ikiwa hali ni kama alivyosema muulizaji, hakuna Talaka, kwa kuwa nia peke yake haipitishi Talaka. Isipokuwa Talaka inapita kwa kufanya moja ya mambo mawili; ima kwa kutamka maneno au kuandika. Au nia peke yake haipitishi Talaka. Kutokana na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu, yanayohadithiwa na nafsi zao maadamu hawajayafanya wala kuyatamka." Nia peke yake wanachuoni wanaona kuwa Talaka haiwezi kupita. Kuwa na utulivu ewe ndugu na umshukuru Allaah kuwa na usalama. Na ninamuomba Allaah Atupe sote Tawfiyq. Swali: Walii wa mwanamke akimuwekea sharti asioe (mwanamke mwingine) juu ya binti yake, kisha akafanya. Je, ni haki kwa mke kuomba Talaka? Imaam Ibn Baaz: Ndio, akimuwekea sharti asioe mwanamke mwingine, sharti ni sahihi kutokana na kauli sahihi ya wanachuoni. Na anaweza kuomba watengane akioa. Na akiendelea kuishi nae, Alhamdulillah. Swali: Mke wangu kwa sasa haswali na wala haswali. Na hii ilikuwa ni sharti yangu kwake kabla ya kufunga nae ndoa. Na baada ya ndoa nikawa nimemwacha kwa kiasi cha muda miezi mitano. Ipi hukumu ya Kishari´ah kwa mke kama huyu? Imaam Ibn Baaz: 58 Mwanamke asiyeswali hazingatiwi kuwa ni Muislamu, bali anazingatiwa kuwa ni kafiri kutokana na kauli yenye nguvu ya wanachuoni. Kwa kuwa kuacha Swalah ni kufuru kubwa, kwa kuwa Swalah ndio nguzo ya Uislamu. Na imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema: "Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao (makafiri) ni Swalah, atakayeiacha amekufuru." Na hili linawahusu wanaume na wanawake. Na kauli yenye nguvu ni kuwa ni kufuru kubwa, hii ndio kauli sahihi na ndio kauli waliokubaliana Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kama alivyosema ´Abdullaah bin Shaqiyq: "Maswahabah wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakuwa wanaona kitu mtu akikiacha ni kufuru isipokuwa kuacha Swalah." Hii ni dalili inaonesha kuwa [Maswahabah] (Radhiya Allaahu ´anhum) walikubaliana juu ya hili. Asiyeswali hana kheri yoyote. Ni wajibu kutengana nae kabisa. َو َ ُ ل ُ َّل هُنَّ حِل ل َّون َلهُن ِ م َي َ ُّحل َ م ْه ْه "Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao." (60:10) Na wala usilale nae katika kitanda kimoja, kwani mwanamke huyu hana kheri yoyote, bali ni wajibu kuachana nae. Swali: Nilioa mtoto wa mjomba wangu nikafunga nae ndoa na wala sikumwingilia. Na mke huyu (niliyemuoa) ni dada wa kaka yangu katika kunyonya, yaani alinyonya kwa mamangu na mimi sikunyonya kwa mama yake. Je, ndoa hii ni Halali au Haramu? Imaam Ibn Baaz: 59 Ndoa hii haina neno. Maadamu yeye hakunyonya kwa mama yako na wewe hukunyonya kwa mama yake, haina neno. Ama kaka yako kunyonya ziwa moja na mke wako, hili halizingatiwi. Muhimu ni kuwa, hili halina neno ewe muulizaji. Swali: Mke wangu mimi haswali. Na nimeshamwamrisha Swalah zaidi ya mara moja lakini hapokei (nasaha). Hali kadhalika havai Hijaab, na nywele zake zinaonekana na watu wote. Naomba unipe faida nimfanye nini? Imaam Ibn Baaz: Mwanamke huyu, kakusanyikiwa na shari mbili kubwa. Na moja wapo ni kubwa zaidi kuliko nyingine. 1) Shari ya kwanza ni kutoswali kwake kwake na hii ni kufuru kubwa kutokana na kauli ya sahihi. 2) Shari yake ya pili, ni kutojisiri kwake kwa Hijaab. Inatakikana kwako na hili ni jambo la wajibu kutengana nae, kwa kuwa haijuzu kwa Muislamu (wa kiume) kubaki na mwanamke kafiri. Anasema (Ta´ala): َو َ ُ ل ُ َّل هُنَّ حِل ل َّون َلهُن ِ م َي َ ُّحل َ م ْه ْه "Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao." (60:10) Ni wajibu kwako kutengana nae maadamu hapokei nasaha. Ni wajibu kuachana nae. Na ninakubashiria kuwa utapata aliye bora kuliko yeye. Na (huyo mwanamke) tunamuombea kwa Allaah uongofu. Muhimu ni kuwa, huyu mwanamke ana shari mbili ambazo ni kubwa, na moja wapo ndio kubwa zaidi kuliko nyingine. Nayo ni kuacha Swalah, hii ni kubwa kwa kuwa hii ni kufuru kubwa. Na kule kutojisitiri kwake si nywele zake wala uso wake, hii pia ni dhambi na shari kubwa. Ni wajibu kwako kutengana nae, kutahadhari nae na kumpa Talaka. Tunamuomba Allaah sote Atupe afya. Na yule mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora 60 kuliko hicho (alichokiacha). Allaah Atakupa aliye mbora na mwema kuliko yeye In Shaa Allaah. Swali: Inajuzu kwa Muislamu kunuia nia mbili kwa wakati mmoja? Kama kwa mfano kunuia Swalah iwe ya Sunnah ikiwa atakosea katika Swalah ya faradhi, au akakosea katika Hajj au Zakaah? Imaam Ibn Baaz: Hatujui kuwa hili lina asli. Bali asli ni salama na afya. Anuie Swalah anayoswali kama anavyotaka; Sunnah ya Dhuhr, Sunnah ya Maghrib, Sunnah ya ´Ishaa, Sunnah ya Dhuhaa bila ya kuwa na mashaka (wasiwasi) aliyoashiria. Asli ni salama. Alhamdulillaah. Na wala hatujui kuwa hili lina asli yoyote ya kuweka nia mbili. Swali: Mimi namwamini Allaah kuwa ni Mmoja asiyekuwa na mshirika, lakini nimesikia watu wakisema kuwa kuna mtu mwenye mavazi meupe sana na hakuonekani kwake athari za safari. Mtu huyu akikupa kitu, basi baraka ya mali yako inazidi. Naomba faida, je, mambo haya yanaingia akilini au ni katika Bid´ah? Imaam Ibn Baaz: Kauli hii ni ya batili na haina msingi wowote. Na mtu kama huyu hapatikani. Na baadhi ya watu wanadhani kuwa aliyekusudiwa hapa ni Khidhr, na hili ni jambo lisilokuwa na usahihi wowote. Khidhr alikufa muda tu kabla ya kuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutokana na kauli ya sahihi ya 61 wanachuoni. Na ukhurafi huu uliyosema, ni katika mambo ya Kishaytwaan na hayana msingi wowote. Inatakikana ujue hilo, na usidanganyike na maneno ya watu hawa wachawi. Swali: Ipi hukumu ya mwenye kunuia kumtaliki mke wake na akachelewesha kufanya hivyo? Imaam Ibn Baaz: Mwanaume akinuia kumtaliki mke wake kisha akaacha hilo na asifanye kitu, Talaka haipiti. Nia haifanyi Talaka kupita. Kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Hakika ya Allaah Kausamehe Ummah wangu yanayohadithia nafsi zao maadamu hawajayafanaya au kuyatamka." Maadamu hajayatamka na wala kuyafanya - kuandika hilo - isipokuwa kaweka nia tu, nia hii haipitishi chochote na mke atabaki katika asli yake. Talaka haipiti mpaka aandike Talaka au aitamke. Swali: Ni sahihi kwa mwanaume kumuosha mke wake anapokufa au msichana wa mwaka moja mpaka miwili hata kama atakuwa ni ajinabi kwake? Imaam Ibn Baaz: 62 Hakuna ubaya wowote mwanaume kumuosha mke wake, na mke kumuosha mume wake kwa kufuata Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kinyume na mke, hapana. Lakini mdogo ni kama mfano wa mke. Hakuna ubaya mwanaume akamuosha msichana mdogo, na wala hakuna neno akamuosha kama mke. Ama mama yake, msichana wake, dada yake na mfano wa hao, haifai kwake kuwaosha. Bali hawa wanaoshwa na wanawake. Lakini msichana ambaye ni mdogo haina neno anaweza kuoshwa na wanaume. Ikiwa ni chini ya miaka saba; kama mfano wa msichana wa miaka mitano, tatu, mine, haina neno. Hali kadhalika, mvulana wa chini ya miaka saba anaweza kuoshwa na wanawake pia. Watoto chini ya miaka saba wanaweza kuoshwa na wanaume na wanawake. Swali: Mwanaume aliyeoa kumwaga manii nje ya tupu ya mwanamke ni Haramu au hapana? Na khaswa anafanya hivi wakati wa hali ya hedhi au damu ya uzazi? Imaam Ibn Baaz: Kumwaga manii nje ya tupu ikiwa kuna manufaa, hakuna neno kufanya hivyo. Na hii huitwa "´Azl". Na imethibiti ya kwamba Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakifanya ´Azl, na akawakubalia hilo (´alayhisSwalaat was-Salaam). Kukiwa na haja ya kufanya ´Azl, bi maana kumwaga manii yake nje ya tupu, ima kwa kuwa mke wake hawezi kushika mimba nyingine wakati ule au kwa sababu aliyoisema muulizaji. Kwa kuwa lililo la Haramu (wakati wa hedhi na nifasi) ni kufanya nae jimaa. Akicheza nae katika tupu yake (mke) na akamwaga manii kwa nje na wala asimjamii, hakuna ubaya kufanya hivyo. Kwa kuwa Haramu ni kufanya jimaa. Kasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusiana na mwanamke wa hedhi: "Fanya kila kitu isipokuwa (kitendo cha) ndoa." 63 Yaani jimaa. Anaweza kukutana nae, kumkumbatia, kucheza nae na kustarehe nae kwa tupu yake, tumbo lake na yasiyokuwa hayo. Lakini bora zaidi, awe na kizuizi kwa juu kama ´Izaar au suruwaliili kujiepusha na khatari. Kwa kuwa mwenye kuikabili tupu, Shaytwaan anaweza kumshawishi kufanya kitendo cha jimaa kilochoharamishwa. Bora, ni yeye (mume) akutane nae nyuma ya ´Izaar, suruwali au kanzu. Anasema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha): "Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiniamuru nijifunge vizuri nguo yangu kiunoni kisha akinikumbatia hata nikiwa katika hedhi." Namna hii ndivyo alivyosema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha). Makusudio ni kuwa, Sunnah kwa upande wa mume ikiwa mwanamke yuko katika hedhi au nifasi, akutana nae nyuma ya ´Izaar au nyuma ya suruwali na mfano wa hivyo. Lakini lau akikutana nae ndani ya ´Izaar na ndani ya suruwali, hakuna ubaya wa hili. Kumekuja katika Sunnah kitu kinachotolea dalili hilo. Kwa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Fanya kila kitu isipokuwa (kitendo cha) ndoa." Ilikuwa ni baada ya kuambiwa kuwa mayahudi pindi mwanamke anapoingia hedhini, basi wanamchukia, wanamtenga na kumhama nyumbani. Ndio akawa amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Fanya kila kitu isipokuwa (kitendo cha) ndoa." Yaani wakhalifuni mayahudi, bi maana fanya kila kitu ila jimaa. Hivyo akiweka tupu yake kwenye mapaja na akaweka nje ya tupu, hakuna ubaya. Lakini asimjamii, ni Haramu kwake kumjamii sawa ikiwa atateremsha au kutoteremsha. Ni wajibu kujiepusha na jimaa. Ama kule kuweka kwake tupu yake kwenye mapaja yake au karibu na tupu yake (mke) mpaka akamwaga bila ya kuiingiza, hakuna ubaya kwa hilo. Lakini lililo bora zaidi kabisa, ni yeye kujiepusha na hili, ili Shaytwaan asimshawishi kufanya kitendo kilichoharamishwa. Na kwa ajili ya hili, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawaamrisha wanawake wajisitiri (tupu zao) wakati wa kukutana nao moja kwa moja (´alayhis-Swalaat was-Salaam). 64 Swali: Mtu kama alikuwa na mke akamtaliki. Je, anaweza kumuoa dada yake ndani ya eda yake (huyo mke wake)? Na akifa anaweza kuoa katika hali hii? Imaam Ibn Baaz: Akimtaliki mke wake, haijuzu kwake kumuoa dada yake wala wanawake wengine isipokuwa baada ya eda, baada ya kwisha kwa eda. Ikiwa ni Talaka rejea, hili wamekubaliana wanachuoni wote. Ya kwamba haijuzu kwake kumuoa dada yake wala mwanamke mwingine yeyote isipokuwa baada ya kwisha kwa eda, kwa kuwa mwanamke rejea ni mke. Ama ikiwa ni Talaka Baain [Talaka ambayo kakosa haki ya kumrejeakwa kuwa eda imekwisha], au Talaka kwa mwanamke kujivua (katika ndoa), hapa kuna tofauti, lakini kauli yenye nguvu ni kuwa asioe mwingine ila baada ya kwisha kwa eda. Ama (mke) akishakufa, hakuna ubaya akaoa mwanamke mwingine baada ya siku moja au mbili tokea siku ile kafariki. Ikiwa mke kafa, eda yake imekwisha kwa kufa kwake, ndoa imekwisha kwa kufa kwake. Katika hali hii, hakuna ubaya akamuoa dada yake au mwanamke mwingine yeyote. Swali: Mimi ninafanya kazi ya uguuzi, na wakati fulani ninawapa wanaume "ibar" kutokana na sheria ya kazini kwa kukosekana muuguzi mwanaume awezae kuwapa "ibar" hii. Na anakuwa mgojwa katika hali nzito ya kuhitajia dawa hii. Ipi hukumu ya hili na je nina madhambi? Imaam Ibn Baaz: Kukihitajia haja (dharurah) ya hilo, hakuna neno In Shaa Allaah. Lakini ni wajibu kwako kuwa pamoja na wanawake. Na wauguzi wanaume wawe pamoja na wanaume wenzao, na kila mmoja achunge na kutimiza kazi yake. Kukitokea dharurah ya wewe kumsimamia mwanaume kwa kukosekana muugizi mwanaume, hakuna neno In Shaa Allaah. 65 Swali: Ipi hukumu ya mwanamke ambaye ametalikiwa kisha akaolewa na mwanaume mwingine. Na baada ya muda mrefu akamuomba yule mume wake wa kwanza kumwandikia Talaka ili kupata pesa kutoka serikali, pamoja na kuwa (mwanamke huyu) kwa sasa yuko katika dhimma ya mwanaume ambaye yuko nae sasa? Imaam Ibn Baaz: Ni kama tulivyosema. Hata kama itakuwa ni kweli katalikiwa, lakini akaficha ukweli ya kwamba kaolewa (na mume mwingine) baada ya hapo, haya ni maovu na utatizi. Ndani yake kuna hila na uadui. A´udhubi Allaah. Kuchukua mali pasina haki ni jambo ovu na ni ulaji wa vya Haramu. Tunamuomba Allaah afya. Swali: Mimi ninawasalimia na mkono watoto wa shangazi yangu na mjomba wangu bila ya kizuizi. Je, hili linajuzu? Na ikiwa haijuzu, je naweza kuweka mkononi mwangu abaya na vifuniko vya mikono (gloves)? Imaam Ibn Baaz: Haijuzu kwa mwanamke kupeana mikono na wanaume ikiwa sio Mahaarim zake; kama mfano wa watoto wa shangazi na mjomba wake, hakika hawa sio Mahram zake. Haifai kwake kupeana nao mikono, sawa ikiwa kwa kuweka kizuizi au bila ya kuzuizi. Isipokuwa anaweza kupeana mikono na Mahaarim zake; kama kwa mfano wa kaka yake, mjomba wake, shangazi yake, baba yake au wanawake wenzake haina neno. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): 66 "Mimi sipeani mikono na wanawake." Mwanaume asipeani mokono na mwanamke, na mwanamke asipeani mikono na mwanaume ambaye sio Mahram wake; kama kwa mfano wa mtoto wa shangazi yake, mjomba wake, jirani yake, mume wa dada yake, kaka wa mke wake. Wote hawa ni watu ajinabi kwake, haifai kwake kupeana nao mikono, sawa iwe kwa kuweka kizuizi au pasina kizuizi. Swali: Ipi hukumu ya kutia wanja? Na je, imethibiti kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba alikuwa anaweka wanja machoni mwake? Imaam Ibn Baaz: Kutia wanja ni Sunnah. Na imethibiti ya kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anatia wanja machoni mwake. Ni Sunnah. Swali: Kuna mtu ana watoto watatu ambao hawana mapungufu katika kumtii na kumtendea wema, na yeye (mzazi huyo) anawaombea dhidi yao. Je, Du´aa yake itawadhuru? Imaam Ibn Baaz: Haimpasi muumini kuomba dhidi ya watoto wake, bali ni wajibu kwake kutahadhari kwa hilo, kwa kuwa anaweza kuomba katika saa ya kujibiwa. Haimpasi kwake kuomba dhidi yao, na ikiwa ni wema jambo hili linakuwa baya zaidi kukosa kuwaombea Du´aa. Ama ikiwa wana mapungufu, haitakikani vilevile kwake kuomba dhidi yao. Bali kinyume chake, awaombee 67 uongofu na wema na Tawfiyq. Namna hii ndivyo inavyopasa kuwa kwa muumini. Na kumekuja nususi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambazo zinatahadharisha mzazi kumuombea Du´aa mbaya mtoto wake, ahli zake na mali yake. Kwa kuwa anaweza kuomba saa ya kujibiwa, akawa amejidhuru nafsi yake mwenyewe, ahli zake na mtoto wake. Inatakikana kwako ewe muulizaji uuhifadhi ulimi wako na umkataze unayemjua kuwa anafanya jambo hili auhifadhi ulimi wake na amche Allaah kwa hilo, mpaka asiombe dhidi ya mtoto wake wala kuwaombea Waislamu wengine. Bali kinyume chake, awaombee kheri, uiamara na msimamo. Na isiwe kuwaombea Du´aa dhidi yao kwa yanayowadhuru. Swali: Muulizaji anasema kuwa mzazi wake kafikisha zaidi ya miaka 85 naye ni mgonjwa hawezi kutia Wudhuu kwa maji. Tunampa udongo atayamamu kwao. Je, inajuzu kwake kutayamamu kwa udongo huu mwezi au zaidi? Imaam Ibn Baaz: Ndio, hakuna neno. Atatumia udongo mpaka katika muda maalumu. Maadamu anapata udongo, Alhamdulillaah. Swali: Kuna mtu kamjamii mwanamke wake ambaye alikuwa anataka kumchumbia kabla ya kufunga ndoa, akambebesha mimba akamwambia hilo walii wa mwanamke. Wakawa wamefunga ndoa kisha Allaah Akawaruzuku mtoto. Ipi hukumu ya mtoto huu Kishari´ah kwa kuzingatia kuwa baba amekubali ni wake? 68 Imaam Ibn Baaz: Mtoto huyu ni wa Zinaa. Kwa kuwa kufanya nae jimaa kabla ya kutimia kwa ndoa, ni jambo ovu na Zinaa. Hatonasibishwa nae na wala hatokuwa mtoto wake (baba), isipokuwa atanasibishwa kwa mama yake, au atanasibishwa kwa ´Abdullaah, ´Abdul-Latwiyf, ´Abdul-Maalik kwa minajili ya kumsitiri katika Mustaqbal. Muhimu ni kwamba, hatonasibishwa kwa baba yake kwa kuwa ni mtoto wa Zinaa, lakini badala yake atanasibishwa kwa mama yake. Ni juu yao wote kufanya Tawbah. Ni juu ya mwanaume na mwanamke watubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na wafunge ndoa upya, kwa kuwa ndoa ilifanywa katika hali ya ujauzito wa Zinaa. La wajibu ni wafunge ndoa upya, baada ya kujifungua. Awafungishe ndoa walii wa mwanamke, baada ya wote wawili kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Swali: Nikiwa ni mwenye kujiheshimu kwa vazi la Kiislamu nyumbani na wala siachi (kuvaa) Khimaar (shela, ushungi) kichwani mwangu. Je, inajuzu kwangu kukaa na watoto wa kiume wa ami na shangazi yangu na mfano wao ikiwa sote ni wanaume na wanawake twakaa sehemu moja? Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya kukaa na watoto wa ami na shangazi pamoja na kuwa na heshima, kujisitiri na kuvaa Hijaab. Hata uso, ni ´Awrah kwa kauli ya sahihi. Ni wajibu fuunika na kichwa, hivyo viwili ni aula zaidi atapokaa na ndugu zake; watoto wa shangazi, mjomba au jirani yake kwa mipaka mizuri ya kidini isiyokuwa na neno ndani yake. Pamoja na kujisitiri, kuvaa Hijaab na wala kutoonesha kitu katika hivyo; si uso wala kingine chochote, hakuna ubaya kwa hilo. Na wala haitoshi kufunika kichwa, bali ni wajibu kufunika uso pia. Mwanamke anatakiwa kujiheshimu na kujiweka mbali na sababu zinazopelekea katika fitina; (asichukulie sahali) si pamoja na watoto wa shangazi yake, mjomba wake wala wasiokuwa wao. 69 Swali: Mimi nina kaka na ndugu ambao kwa masikitiko makubwa hawaswali na wala hawasimamishi mipaka ya Allaah. Je, ni lazima juu yangu kuwakata? Kila ninapowaamrisha mema au kuwakataza maovu, wanafanya mzaha na maskhara na mimi na wanasema "je wewe unataka kuwafanya watu wote kuwa wema?" Wao wamekataa kukaa na mimi na wamenikata, lipi la wajibu kwangu kufanya juu yao? Imaam Ibn Baaz: Ni juu yako kuwahama na kuwakata. Maadamu hawakubali nasaha na hawaswali, inatakikana kwako kuwahama na kuwakata mpaka hapo Allaah Atapowaongoza. Hili ndilo la wajibu, bali hii ndio Sunnah iliyosisitizwa. Baadhi ya wanachuoni wanaona hivi, uwajibu wa kuwahama na kuwakata kutokana na upotofu wao na kuzuia njia za kheri. Lakini ukiwasiliana nao baadhi ya nyakati kwa kutaraji pengine Allaah Akawaongoza, kwa kuwalingania na kuwapa nasaha, hakuna neno. Na ikiwa wataendelea, hakuna neno kwako kuwakata na kujiweka kwako mbali nao kikamilifu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakata Maswahabah watatu wakati walipoacha kwenda kupigana vita pamoja naye bila ya udhuru. Muhimu ni kuwa, watu hawa inatakikana kuwahama. Kwa uchache, kuwahama kunakuwa ni Sunnah iliyosisitizwa mpaka hapo Allaah Atapowaongoza na kuwarudisha katika usawa. Swali: Kijana anapotaka kumposa mmoja katika wasichana. Katika hali hii, je ni wajibu kwake (kijana huyo) kumuona? Na je, ni sawa msichana huyo kufunua kichwa chake ili abainishe uzuri wake zaidi kwa mposaji wake? 70 Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya, lakini sio wajibu bali ni jambo limependekezwa. Ni jambo limependekezwa (kijana huyo) akamuona na yeye (msichana huyo) akamuona (mvulana huyo). Kwa kuwa hii ni njia ya karibu ya kukubali. Mtume (´alayhis-Salaam) kamwamrisha mwenye kutaka kuchumbia atazame (kwanza). Akifunua uso wake, na miguu yake na kichwa chake, haina neno kutokana na kauli sahihi. Wamesema baadhi ya wanachuoni kuwa inatosha uso wake na vitanga vyake, lakini kauli ya sahihi ni kuwa haina neno kufunua kichwa na miguu atazame apendekezwe na uzuri wake. Wanaweza kutazamana (kwa kuwepo walii wa mwanamke)kwa kuwa hii ni njia ya karibu ya kuweza kukubali. Hili liwe pasina mchanganyiko (yaani wasiwe wao wawili tu), bali wawe pamoja na baba yake na msichana, au kaka yake au mwanamke mwingine. Wasichanganyike wao wawili tu. Swali: Kuna kijana ambaye anataka kuoa msichana ambaye hajui kuwa anaswali au hapana. Je, ndoa hii inajuzu na ipi hukumu ya hilo? Imaam Ibn Baaz: Ni lazima kuthibitisha kwanza jambo hili. Aulizie kwanza, kwa kuwa kumuoa mwanamke ambaye ni kafiri haijuzu. Kwa Kauli Yake (Subhaanah): َو َ ُ ل ُ َّل هُنَّ حِل ل َّون َلهُن ِ م َي َ ُّحل َ م ْه ْه "Wao si (wake) halaal kwao (hao makafiri), na wala wao si (waume) halaal kwao." (60:10) Na mwenye kuacha Swalah anakufuru, kutokana na kauli ya sahihi ya wanachuoni hata kama atakuwa anakubali uwajibu wake. Akiacha kwa uvivu na kuzembea anakufuru. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Baina ya mtu na Shirki au kufuru ni kuacha Swalah." 71 Na kasema tena (´alayhis-Swalaat was-Salaam): "Ahadi iliopo baina yetu sisi na wao ni Swalah, atakayeiacha amekufuru." Ikiwa haswali haijuzu kumuoa. Ama akijua kuwa anaswali vizuri, anaweza kumuoa. Kasema Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Mwanamke anaolewa kwa mambo mane: "Kwa mali yake, uzuri wake, nasabu yake na Dini yake, basi shikilia (chagua) mwenye sifa za Dini utasalimika." Kumchagua mwanamke mwenye Dini ni jambo limefaradhishwa. Na katika Dini jambo muhimu na nguzo kubwa ni Swalah inayokuja baada ya Shahaadah mbili. Swali: Je, ni wajibu kupandisha mikono wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam tu au ni lazima kuipandisha katika nguzo zote za Swalah? Imaam Ibn Baaz: Sunnah ni kupandisha mikono wakati wa Ihraam, na wakati wa Rukuu´, na wakati wa kutoka katika Rukuu´ na wakati wa kusimama kutoka katika Tashahhud ya kwanza mpaka ya tatu. Na hilo sio wajibu bali ni Sunnah. Lilifanywa na Mtume (´alayhi-Salaam), Makhalifah waongofu na lilinukuliwa kutoka kwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Sunnah ni muumini mwanaume na mwanamke afanye hivyo katika Swalah zake zote. Kwa kuwa asli ni kuwa, mwanamke ni sawa na mwanaume katika Ahkaam isipokuwa kwa yale yaliyokhusishwa na dalili. Sunnah ni kunyanyua mikono yake katika Takbiyrah ya kwanza mpaka kwenye mabega au masikio yake, hali kadhalika (apandishe) mikono yake wakati wa Rukuu´ na wakati wa kuinuka kutoka katika Rukuu´, na hali kadhalika wakati wa kuinuka kutoka katika Tashahhud ya kwanza mpaka ya mwisho. Kama ilivyokuja katika khabari zilizo sahihi kutoka kwa Mtume 72 (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Na hili ni jambo Mustahabah na Sunnah na sio wajibu. Na lau ataswali bila ya kupandisha, Swalah yake ni sahihi. Swali: Ipi hukumu ya kuwatahiri wasichana? Kwetu ni lazima tufanye hivyo, na kuna baadhi ya watu wamenambia kuwa ni jambo lisilojuzu kwa kuwa ndani yake kuna kama kuadhibu. Ipi hukumu ya hilo? Imaam Ibn Baaz: Kutahiriwa (kwa wanawake) ni Sunnah iliyosisitizwa, hali kadhalika kwa wanaume, wote ni Sunnah iliyosisitizwa. Na kuna kundi la wanachuoni ambao wanaona ni wajibu kwa wanaume na ndio kauli yenye nguvu. Inatakikana kuwatahiri wanaume na wala haitakikani kulichukulia sahali, na namna hii ni kuwa imependekezwa kuwatahiri wanawake ikiwa atapatikana mwenye kujua hilo katika wanawake wanaotahiri. Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali Rakaa ngapi baada ya Swalah ya Ijumaa? Tunaomba faida. Imaam Ibn Baaz: Masru´ah ni kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali baada ya Ijumaa Rakaa mbili nyumbani kwake. Namna hii ndivyo ilivyokuja katika Swahiyh al-Bukhaariy na Muslim, Hadiyth ya Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa). "Alikuwa akiswali Rakaa mbili baada ya Ijumaa nyumbani kwake." 73 Lakini, kasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Mwenye kuswali baada ya Ijumaa, aswali (Rakaa) nne." Wanasema wanachuoni, kuoanisha baina ya Hadiyth hizi mbili ni kuwa, akiswali Msikitini ataswali Rakaa nne, na akiswali nyumbani kwake ataswali Rakaa mbili. Kuoanisha baina ya nususi hizi mbili. Swali: Nilioa mwanamke nikabaki nae kwa muda, kisha nikamtaliki na akaolewa na mwanaume mwingine baada yangu. Je, inajuzu kwake kumbusu na kumsalimia baba yangu baadaya kumtaliki? Imaam Ibn Baaz: Hakuna ubaya. Kwa kuwa Allaah Kasema: ُئ َح ُ ئ م ِ ل أَ ْب َنا ِ َل َ و َ ُك "Na (mmeharamishwa) wake wa watoto wenu." (04:23) Ni katika wake wa watoto (walioharamishwa kwa baba). Hata kama amemtaliki. Ni Mahram wa baba yako. Muulizaji: Yaani umahram wao ni wenye kubaki hata kama amemtaliki? Imaam Ibn Baaz: Ni kama mke wa baba yake, lau baba yake atamtaliki, bado (mama huyo) ataendelea kuwa Mahram wake (mtoto). Allaah Kasema: ِّ ِّن ال ُ ُح آ َباؤ َو َ ما َن ء ِ ل َتن َ ن َ كم م َ ك َ كحُوا َ ِ سا 74 "Na wala msiwaoe (wake) waliowaoa baba zenu." (04:22) Baba akimtaliki (mke wake) au mtoto (mke wake), anakuwa ni Haraam (huyu kwa yule, na yule kwa huyu). Swali: Mimi nimeoa wanawake wawili, lakini wote wawili hawaswali, wanafunga tu mwezi wa Ramadhaan. Nimeshawaamrisha Swalah zaidi ya mara moja. Mmoja wao aliswali siku kadhaa, na pindi niliporejea Misri nikitoka Saudi Arabia nikakuta ameacha Swalah. Na (mke) wa pili anasema hajui kitu katika Qur-aan hata al-Faatihah. Nifanye nini? Imaam Ibn Baaz: Ni juu yako uwafanye watubu na uwabainishie umuhimu wa Swalah na kwamba ndio nguzo ya Uislamu na kwamba kuiacha ni kufuru, wakitubu Alhamdulillaah ubaki nao. Na ikiwa hawakutubu, ni wajibu kwako kutengana nao na Allaah Atakupa walio bora kuliko wao. "Mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora kuliko hicho." Na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema: ُ حي ْز ْم َ ْث ُ ْو َير َّ من َي ُل َيحْ َتسِ ب ُق ُ َّعل ل َ ْه مِن َ رجً ا َخ َ ه َ ْه َيج َ ق اللَّـ َو َ ِ ت "Na yeyote (yule) anayemcha Allaah Atamajaalia njia (ya kutoka katika matatizo). Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii." (65:02-03) Na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema: َ َّ من َي ُ َّعل ل ه يُسْ رً ا ِر َ ْه َيج َ ق اللَّـ َو َ ِ ت ِ ْه مِنْ أم "Na yeyote (yule) anayemcha Allaah Atamjaalia wepesi katika jambo lake." (65:04) Ni wajibu kwako uwafunze, uwafunze al-Faatihah na Suurah fupi katika nyakati ambazo nyoyo zitakuwa zimetulia, uwafunze na ujitahidi kwa hilo na 75 wewe utakuwa mwenye ujira mkubwa. Wakishindwa kusoma al-Faatihah, walete badala yake Adhkaar; kwa kusema "Subhaanallaah","Alhamdulillaah", "Laa ilaaha illa Allaah", "Allaahu Akbar" na "Laa Hawlah wa laa Quwwatah illa billaah". Mtume (´alayhis-Salaam) kaamrisha asiyeweza al-Faatihah alete Dhikr hizi. Akishindwa, alete Dhikr hizi. Lakini iwe ni pamoja na kujaribu katika nyakati za mbele kuihifadhi (al-Faatihah) na kujifunza nayo. Muulizaji: Kuwafanya kwake watubu ni kwa ajili ya kuacha kwao Swalah? Na ikiwa hawakutubu, ni juu yake kufarakana nao? Imaam Ibn Baaz: Ndio. Imaam Ibn Baaz: Mpaka hapa tumepata kujua kuwa, kusherehekea Maulidi ya Mtume ni Bid´ah bila ya shaka. Na ni wajibu kuiacha na wala haijuzu kuifanya. Na yule atakayeyafanya, yuko baina ya mambo mawili: 1) Ima ni mjinga hajui haki, afunzwe na kuongozwa. 2) Au ni mwenye kasumba za kufuata matamanio na kiburi. Alinganiwe katika usawa na aombewe uongofu na Tawfiyq. Na katika watu wote hawa wawili hakuna mwenye hoja, sawa huyu wa kwanza ambaye ni mjinga wala huyu wa pili mwenye kasumba. Wote hawana hoja. Hoja inapatikana katika Aliyosema Allaah na Mtume Wake. Na sio katika kauli isiyokuwa ya hao wawili. Kisha kusema kuwa Bid´ah imegawanyika sehemu mbili; Bid´ah nzuri na mbaya, na katika Haramu na wajibu, huku ni kutoa kauli pasina dalili. Na wameliradi hilo Ahl-ul-´Ilm wal-Yaqiyn na kubainisha makosa ya mgawanyo huu. Na wametumia dalili kwa kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Atakayezusha katika Amri yetu hii yasiyokuwemo, basi yatarudishwa." (Muttafaq) 76 Na Imaam Muslim kapokea katika Swahiyh yake, Hadiyth kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anha)ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema: "Atakayefanya ´amali isiyokuwa humo na Amri yetu, basi itarudishwa." Na katika Swahiyh, Hadiyth kutoka kwa Jaabir (Radhiya Allaahu ´anhu) ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikhutubu siku ya Ijumaa akisema: "Amma ba´ad: "Hakika maneno bora ni Kitabu cha Allaah, na uongofu bora ni wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), na shari ya mambo ni mambo ya kuzua na kila Bid´ah na upotofu." Na wala hakugawa na kusema: "Kuna Bid´ah hii na hii." Bali kasema: "... kila Bid´ah ni upotevu". Bali alizidi kusisitiza hilo kwa kusema: "Tahadharini na mambo ya kuzusha! Hakika kila kitachozushwa ni Bid´ah, na kila Bid´ah ni upotevu." Na Bid´ah inakuwa katika mambo ya Dini ambayo ni ya kujikurubisha na si katika mambo ya dunia. Ama mambo ya dunia; katika mambo ya kula na kunywa, kukafanywa chakula maalumu na cha aina mbalimbali, hili halina neno. Bali kinachozungumziwa ni katika mambo ya kujikurubisha na mambo ya ´Ibaadah ambayo mtu anajikurubisha kwayo kwa Allaah, hapa ndio mahala pa kuzua. Hali kadhalika, uvumbuzi wa mambo na vifaa vya vita; wanaweza kuzua mambo mbalimbali katika silaha za kijihami na kujitetea, hili halina neno. Kinachozungumziwa ni katika mambo ambayo mtu anajikurubisha kwayo kwa Allaah, na ambayo yanachukuliwa kwa watu kuwa ni ukurubisho na ni utiifu kwa Allaah, wakitarajia kwa hayo thawabu kutoka kwa Allaah. Hapa ndipo panapozingatiwa. Yale ambayo hayakufanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala Maswahabah wake na wala hakulitolea dalili (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kuliashiria, bali limezua watu na na kulitia katika Dini ya Allaah, hilo ni Bid´ah. Sawa ikiwa fulani atapenda au atachukia. Na haki ndio yenye haki kufuatwa. Katika mlango huu kuna mengi 77 yamezushwa na watu; kama ya kujenga Misikiti katika makaburi na kuyawekea kuba, hizi ni Bid´ah ambazo zimezua shari nyingi. Mpaka imejitokeza Shirki kubwa na kufikia makaburi kuabudiwa badala ya Allaah kwa sababu ya Bid´ah hii (ya Maulidi). Ni wajibu kwa Muislamu atanabahi na kushikamana na Aliyoyawekea Allaah Shari´ah, na atanabahi na waliyozusha watu na atahadhari nayo. Swali: Anasema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali". Kinachofahamika katika Hadiyth hii ni kuwa, hakuna tofauti kati ya Swalah ya mwanaume na ya mwanamke. Sawa katika kusimama, kuinama, Rukuu´ wala Sujuud. Kwa ajili hii, mimi huwa sitofautishi, lakini huku kwetu baadhi ya wanawake Kenya wananikasirikia na kunambia kuwa Swalah yangu sio sahihi kwa kuwa inafanana na Swalah ya mwanaume. Na wanataja dalili ambazo - kwa mtazama wao - zinatofautisha Swalah ya mwanaume na ya mwanamke; kama kuweka mikono juu ya kifua au kuiacha na namna ya kushutama katika Rukuu´ na yasiyokuwa hayo katika mambo ambayo sikukinaika nayo. Naomba unibainishie; je, Swalah ya mwanaume na ya mwanamke katika utekelezaji kuna tofauti? Imaam Ibn Baaz: Uliyosema dada muulijizaji, sahihi ni kuwa hakuna tofauti kati ya Swalah ya mwanamke na Swalah ya mwanaume. Na waliyosema baadhi ya wanach-uoni ya utofautishaji hayana dalili. Na Hadiyth uliyoisema katika swali lako, nayo ni kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali". Inahusu watu wote. Shari´ah za Kiislamu zinawahusu wanaume na wanawake, isipokuwa yaliyo na dalili ya ukhusishaji. Sunnah ni mwanamke kuswali kama anavyoswali mwanaume; sawa katika Rukuu´, Sujuud, usomaji, 78 uwekaji wa mikono juu ya kifua, hivi ndio bora. Hali kadhalika, jinsi ya kufanya Rukuu´, jinsi ya kufanya Sujuud katika ardhi, yanayosemwa katika Rukuu´ na Sujuud, baada ya kutoka katika Rukuu´ na Sujuud ya kwanza, yote haya (mwanamke) ni sawa kama anavyofanya mwanaume.Kwa kuifanyia kazi dalili ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): "Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali". (Swahiyh al-Bukhaariy) Muulizaji: Kuhusiana na kudhihirisha kisomo na kukimu Swalah, je, Swalah ya mwanamke siinatofautiana na ya mwanaume katika hili? Imaam Ibn Baaz: Kukimu kunatoka nje ya haya, ´Iqaamah na adhaana ni khususan kwa wanaume tu. Kuna maandiko ya haya. Wanaume wanaadhini na wanakimu, ama wanawake hawana kukimu wala kutoa adhaana. Ama kudhihirisha (yaani kusoma kwa sauti) anaweza kusoma kwa sauti; Fajr, Maghrib na ´Ishaa. Rakaa mbili za asubuhi, na Rakaa mbili za mwanzo za Maghrib na ´Ishaa anaweza kusoma kwa sauti kama wanavyofanya wanaume. Swali: Vipi mwanamke anatakiwa kujisitirina Hijaab? Je, ni mwili wake wote? Je anaweza kuonesha vitanga vyake vya mikono na uso wake kwa Mahram zake wote? Imaam Ibn Baaz: Mwanamke anatakiwa kujisitiri kwa watu ambao sio Mahram zake; jirani yake, watoto wa ami yake, mume wa kaka yake. Ama Mahram zake si lazima awe na na Hijaab; hakuna neno akaonesha uso wake, vitanga vyake na miguu yake kwa Mahram zake; kama kaka yake, ami yake na yake, hakuna ubaya. 79 Muhimu ni yeye kujisitiri mbele ya watu ajinabi; kama kwa mfano mtoto wa mjomba wake, kwa kuwa ni ajinabi kwake na sio Mahram. Na kama kwa mfano mume wa dada yake, kaka wa mume wake, ami wa mume wake na mfano wa hawa. Watu hawa ni juu yake kujisitiri mbele yao mwili wote; kuanzia uso mpaka chini. Kwa Kauli ya Allaah (Ta´ala): ْ َم أ َٰ ۚ َ ِوإ ُ وب ُ ِذل ُ سأ َ ْل ۚ ِجاب َ م َتاعً ا ُه َّهن َ م َط َ ءح َو َ فاسْ أَلُوهُنَّ مِن َ َّتمُوهُن َ ذا َ ِ را ْك ْك ِ وب ِ ُوقُل ِ ُر لِقُل "Na mnapowauliza (wake zake) haja, waulizeni nyuma ya pazia. Hivyo ni utwaharifu zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao." (33:53) Anasema tena (Subhaanah): َّ ِزي َن َتهُنَّ إ َو ُ ء ُ ِل ل ُ ل َِّهن َ ي ْبد َ ِ ِهنَّ أَ ْو آ َبا ِ بعُولَت ِ ِهنَّ أَ ْو آ َبائ ِ بعُو َلت ِ ِين "Na wasidhihirishe mapambo yao isipokuwa kwa waume zao, au baba zao, au baba za waume wao... " (24:31) Hivyo ni kuwa, kaamrishwa kujisitiri kwa Hijaab kwa watu ambao sio Mahram zake. Chanzo: http://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177 1420-01-27/1999-05-13